Pages

MKUU WA WILAYA ILALA MH. SOPHIA MJEMA APONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA CHUO CHA ST.MARK KATIKA KUELIMISHA JAMII


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akizungumza na wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Peter Kopweh na kushoto ni Mshauri wa majeshi ya akiba Chripin Makota.

Wanajumuiya ya Chuo cha St. Mark kilichopo Buguruni Malapa wakimsikilia Mh.Sophia Mjema alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akianza ziara kuzuru maeneo mbalimbali yaliyopo katika mazingira ya chuo cha St.Mark akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na timu ya wataalamu wa wilaya ya Ilala.

Na Dickson Mulashani

Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema amekipongeza Chuo cha St Mark (Chuo Kikuu Kishiriki Cha St Joseph) kwa jitihada za kutoa elimu bora kwa manufaa ya wilaya na Taifa kwa ujumla alipofanya ziara ya kikazi chuoni hapo mwishoni mwa juma.

Akiwasili chuoni hapo Mh. Sophia Mjema alikuwa ameambatana na ujumbe wa timu ya wataalam 

katika ngazi mbalimbali a wilaya ya Ilala akiwemo Mratibu Mwadamizi wa Polisi, Mshauri
wa Majeshi ya akiba, Mratibu wa Magereza, Mhandisi , Afisa uhamiaji, Afisa 
Elimu Taaluma, Afisa mipango miji, Afisa ustawi wa jamii, Afisa wa Benki ya 
NMB, Afisa Tarafa, Diwani pamoja na Mwenyekiti wa mtaa.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. Mark Dr.Peter Kopweh akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa wilaya alipokuwa akizuru maeneo mbalimbali katika chuo hicho.



Akimkaribisha mgeni huyo, kaimu Mkuu wa Chuo Dr.Peter Kopweh alianza kwa kuelezea historia fupi ya chuo hicho kilichopo eneo la Buguruni Malapa jirani na shule ya msingi viziwi, kuwa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha St. John’s chenye makao yake makuu mjini Dodoma ambacho kinatoa kozi katika ngazi astashada na shahada za sanaa katika elimu, utawala wa biashara, rasilimali watu, elimu na biashara pamoja na theolojia mathalani shahada ya uzamili katika elimu hili kwa ushirikiano na kampasi mama ya Dodoma.



Sambamba na ukaribisho huo Dr. Kopweh hakusita kuelezea Changamoto zinazokikabili chuo hicho zikiwemo za miundombinu ya barabara, usalama wa mali pamoja na wadau wake kadhalika suala la mipaka ambayo inaonekana kuingiliwa na wakazi wanaozunguka chuo hicho.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mipango Miji Ilala Bw. Benjamin Chagula wakati akiangalia namna ya kutatua Changamoto ya mipaka ya chuo hicho inaingiliwa na wananchi wanaoishi eneo jirani. Nae katika  hotuba yake Mh.Mjema ambaye alipata fursa ya kuzungukia maeneo kadhaa chuoni  hapo alieleza lengo kuu la kufika chuoni hapo kadhalika kupongeza uongozi wa chuo hicho kwa jitihada zinazofanyika.


“Nimeamua kutoka na kuja kuwaona kwani nauthamini sana uwepo wenu katika wilaya yangu (Ilala) kwani hii ni fursa muhimu ya serikali kuwatumia wasomi hata waliopo vyuoni kutatua Changamoto katika maeneo waliyopo, mimi nakazia hapa wilayani na naamini ujio huu utakuwa wenye tija sana kwetu sisi pamoja nanyi kama taasisi katika kushirikiana” alisema Mh. Sophia Mjema.

Kadhalika akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa chuo hicho, Mh.Mjema alitangza kufungua milango ya fursa kwa wasomi hao kufika ofisini kwake na kuleta mawazo pamoja na nguvu zao ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele huku akikazia suala la uzalendo pamoja na wito wa Mh Rais Magufuli kuhusu kufanya kazi.
Vilevile Mh. Mjema alikazia suala la kuimarisha misingi ya elimu ya juu kwa kuwekeza kwenye uboreshaji wa teknolojia kwani dunia ya sasa mitandao umekuwa nyenzo muhimu ya kupata taarifa za kitaaluma.


“Mkakati wa 
kusambaza huduma ya  intaneti (WIFI) 
katika vyuo vikuu hapa Ilala unaendelea kwa kasi na umesimama kwa muda kutokana 
na hali ya mvua lakini baada ya hali hii kila kitu kitakuwa kama 
ilivyoahidiwa,lazima msome kisasa” alihitimisha.


Nae Rais wa 
chuo kwa niaba ya wanafunzi wote alifikisha Changamoto zinazowakabili ikiwemo 
suala la mikopo pamoja na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kwani 
limekuwa likidhohofisha maendeleo ya taaluma alitoa shukrani kwa mkuu wa wilaya 
na kuahidi ushirikiano na ofisi ya wilaya pamoja na kujitoa kutumia taaluma zao 
ndani ya jamii kwa ujumla.


Akihitimisha 
zoezi hili pamoja na kumshukuru Mh.Mjema kwa kufika chuoni hapo, Kaimu Mkuu wa 
Chuo alitoa wito kwa watanzania kujiunga na Chuo hicho hasa wakati huu ambapo 
milango ipo wazi kwa wanafunzi kudahiliwa vyuoni moja kwa moja huku akiwaondoa 
hofu wale wanaobanwa na kazi kuwa watapata fursa ya kusoma masomo ya jioni.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)