Pages

KILIMANJARO DIALOGUE ISNTITUTE YAENDESHA MDAHALO WA MAZINGIRA MANISPAA YA ILALA


Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Bi.Esther Masomhe, (kulia), akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya meza ya duara kuhusu mazingira kwenye Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Juni 5, 2017, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya mazingira duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute iliyoandaa majadiliano hayo, Bw. Habib Miradji.

NA  KVIS BLOG/Khalfan Said
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imesema iko kwenye mkakati mkubwa wa kutengeneza  bustani za kupumzika wananchi na tayari wameanza kuboresha maeneo hayo kwa  kuanzia na eneo bustani ya Samora (Kaburi la Sharif), barabara ya Samora. Akizungumza  kwenye mdahalo wa mazingira uliotayarishwa na Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue  Institute ya jijini Dar es Salaam leo Juni 5, 2017, Afisa Mazingira wa Manispaa 
hiyo, Bi.Esther Masomhe, alisema, pamoja na vipaumbele vingi ambavyo Manispaa  hiyo inakabiliwa navyo, lakini moja ya hatua inazochukua ni kupendezesha jiji,  (City beatification).

“Kuna  maeneo tayari tumeanza nayo kama vile bustani ya Samora pale kaburi la Shariff,  barabara ya Samora, bustani ya Mnazi Mmoja namba mbili eneo laMcahfukoge,  tunakusudia kuiboresha bustani hiyo ili wananchi wapate mahala pazuri pa  kupumzika.” Alisema Bi.Masomhe.

Akifafanua  zaidi alisema, Wilaya ya Ilala ndiyo kitovu cha jiji la Dar es Salaam hivyo  Manispaa inachukuajuhudi mbalimbali kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa katika  muonekano mzuri kwa kuboresha mazingira na bustani zake. Aidha  Afisa huyo wa Mazingira wa wilaya ya Ilala alisema, kwa kuzingatia kauli mbiu  ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, ““Hifadhi Mazingira, kama Muhimili wa  Maendeleo ya Viwanda

“kauli  mbiu hii ina maana kuwa viwanda vingi hapa nchini vimejengwa bila kuzingatia  uhifadhi wa mazingira, utakuta mtu mwenye kiwanda, anashindwa kuhifadhi maji  taka anayozalisha na badala yake anatiririsha kwenye mito, ambako huko kuna  viumbe hai, sihilo tu lakini pia kuna watu wanaendesha kilimo cha mboga mboga,  kwa vile maji wanayotumia ni hayo hayo ya mto ambayo tayari yanakuwa  yamechanganyika na maji taka ya viwandani, walima bustani hutumia maji hayo  kunyweshea bustani zao na hivyo kuwalisha wananchi mboga mboga zenye kemikali, nah  ii ni hatari kwa afya,” alisema Alisema  kwakuwa sheria zipo wazi, watasimamia sheriahizo kikamilifu ili kuhakkiikisha  kiwanda kitakachoanzishwa kwenye Manispaa knazingatia uhifadhi wa mazingira.

Naye  Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya  Kilimanjaro Dialogue Institute, Bw. Habib Miradji amesema, “hakuna mtu ambaye  hafahamu umuhimu wa mazingira, lakini kumekuwepo na tatizo kubwa la  kimazingira, sisi tunaetembea dunia tunaona kuna milima misitu ya asili na  mbuga, kwa kweli inabidi ukae ufikirie jinsi maliasili ilivyotunzwa,  lakini hapa kwetu,  vitu kama hivi havipo,  ilikuwa zamani tu maana hata milio ya ndege na miti asili imetoweka.” Alisema. Bw.  Miradji alihoji nini mikakati ya Manispaa katika uhifadhi wa mazingira kwani  maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu hususan uswahilini, (urbanslams) haya yanakuwa na ongezeko la watu kwa   haraka, familia moja inawezakuwa na watu 10 na zaidi, nini mkakati ya Manispaa 
katika kukabiliana na misongamano ya watu?

Akijibu  hoja hiyo Bi. Masomhe alsiema, kumekuwepo na mikakati mbalimbali ikiwemo ya  utoaji elimu mashuleni, kupitia klabu za mazingira za shule, lakini pia  kuboresha miundombinu kwenye maeneo hayo na kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo  hayo kupitia kwa maafisa afya wa Manispaa ambao hutembelea mara kwa mara ili  kutoa elimu ya usafi wa mazingira.
 Bi.Esther Masomhe, akizungumzia mikakati ya Manispaa yake kuhusu mazingira na utunzaji wake
 Mwenyekiti wa mdahalo huo, ambaye pia ni mdhamini wa taasisi hiyo ya
Kilimanjaro Dialogue Institute, (KDI), Bw. Habib Miradji
 Mshauri wa masuala ya vyombo vya habari, Bw. Felix Kaiza akisikiliza kwa makini mjadala huo.

Katibu  Mkuu wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue Institute (KDI), Bw.Hassan Mzighani,  (kulia), akizungumza kwenye mdahalo huo ambapo alisema anasikitishwa na jinsi  Manispaa inavyoshindwa kudhibiti maji taka, yakiwemo yale yanayosababishwa na  mvua na kutolea mfano nchi kama Norway, ambayo hupata mvua muda mwingi lakini  sio rahisi kukuta barabara au makazi ya watu yakiwa yamezingirwa na maji.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)