Pages

Benki ya UBA yawavutia wateja katika maonyesho ya Sabasaba

 Afisa wa Bank ya UBA Tanzania, Bi Mtinta Joseph Ringa pamoja na afisa wa bank Bw. Sihika Malunguja wakifurahi kumuhudumia mmoja wa wateja aliyetembelea banda la bank ya UBA Tanzania katika Maonyesho ya 41 ya kibiashara Tanzania yaliyoanza hivi karibu. Bank ya UBA inawakaribisha wateja wote kuweza kufika katika banda lao kwaajili ya kujipatia huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo na kufungua akaunti na kujipatia kadi mpya ya Mastercard ambayo unaweza kuwa nayo bila kuwa na akaunti.
 Afisa wa benki ya UBA Tanzania, Bw Fahimu Zuberi akimpatia maelezo kuhusiana na kadi mpya za mastercard mmoja wa wateja waliotembelea banda la benki hiyo lililopo katika banda la Sabasaba kwenye maonyesho ya 41 ya kibiashara ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam
 Afisa wa benki ya UBA Tanzania, Bw Fahimu Zuberi akiendelea kumpatia maelekezo ya kina kuhusiana na kadi mpya mpya za mastercard ambazo mteja anaweza kuwa nayo bila kuwa na akaunti ya benki
Wafanyakazi wa benki ya UBA Tanzania waliopo kwenye banda lao katika maonyesho ya 41 ya kimataifa ya biashara wakiwa katika picha ya pamoja huku wakifurahia kuwahudumia baadhi ya wateja waliofika katika banda lao huku wakiwakaribisha wateja kufika katika banda lao na kujipatia huduma mbalimbali za kibenki. Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)