Msanii nyota wa filamu Tanzania, ambaye pia ni balozi wa Biko, Kajala Masanja, akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 10 aliyoshinda mkazi wa Mwanza, Pildas Emmanuel katika mchezo wa kubahatisha unaoendeshwa na Kampuni ya Biko Tanzania. Droo hiyo ilichezeshwa jana, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI
wa Mwanza, Pildas Emmanuel ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 10 kutoka
kwenye shindano la ‘Ijue Nguvu ya Buku’ katika droo iliyochezeshwa jana jijini
Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na msimamizi wa Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Droo ya
bahati nasibu hiyo inayoendeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi katika
simu za mikononi kupitia huduma za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa ambapo pia
ilichezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema
kwamba droo hiyo imeshirikisha washiriki zaidi ya 10,000 Tanzania nzima na
kufanikiwa Emmanuel kutoka Mwanza kunyakua fedha hizo na kuingia katika
historia ya mshindi wa kwanza kutoka mkoani.
Alisema
Biko wamefurahia kuona mshindi wa droo ya tatu ametoka mkoani, baada ya droo
mbili za awali ambazo zote washindi wake walitoka jijini Dar es Salaam kwa
Christopher Mgaya na Nichoulas Mlasu kuibuka na Milioni 10.
“Tunawapongeza
washiriki wote wanaogombania gurudumu la mchezo wetu wa Biko ambao umeshika
kasi, huku nikimpongeza pia mshindi wetu wa mkoani Mwanza, Emmanuel kuibuka na
ushindi huu ambao kwa hakika unaweza kubadilisha maisha yake.
“Bado
kila mtu anaweza kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 10 kwa droo ya wiki pamoja na
zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000
500,000 na Milioni moja kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala
kwenye simu zao za mikononi huku namba yetu ya kampuni ikiwa ni 505050 na namba
ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.
Naye
Emmanuel alisema bado haamini ametangazwa kushinda zawadi hiyo inayoweza
kumfanya atimiz ndoto zake za kimaisha kwa kuhakikisha kwamba fedha hizo
anazitumia vizuri endapo atakabidhiwa kutoka Biko, huku akikiri kuwa ametokea
kuupenda mchezo wa Biko.
“Nimekuwa
nikicheza Biko kwa sababu ni mchezo mzuri maana hauna mlolongo mrefu, hivyo
wakati nasubiria zawadi yangu kutoka Biko, nawashauri Watanzania wote
kugombania gurudumu la Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda donge nono,”
Alisema.
Baada
ya kutangazwa kunyakua Sh Milioni 10, mshindi huyo anatarajiwa kukabidhiwa
fedha zake mapema wiki hii kwa utaratibu wa kufunguliwa akaunti katika benki ya
NMB sambamba na kupewa elimu ya kifedha kama walivyopatiwa washindi wenzake wa
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)