Pages

WATEJA WA AIRTEL LAKI NNE WAJISAJILI KUPATA HUDUMA ZA AFYA BURE


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na programu ya mHealth Tanzania PPP (mHealth Tanzania Partnership) inayoratibiwa na Cardno Tanzania chini ya ), ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto kupitia mradi wa Wazazi Nipendeni wawawezesha wamama wajawazito na wenye watoto wadogo takribani laki 4 kujiunga na kupata taarifa mbalimbali za afya kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu bila malipo yoyote pindi wanapojiunga na kupata jumbe hizi kupitia simu zao za mkononi.

Mradi huo wa Wazazi Nipendeni ulioko chini ya Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto umeanzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya afya na kuokoa vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano ambavyo vilikuwa vinakuwa kwa kasi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na elimu ya kutosha juu wa maswala ya kiafya.

Akitoa tathimini juu ya mradi huo mpaka sasa Bwn Mtasingwa Saulo kwa niaba ya mHealth Tanzania Partnership alisema” mHealth Tanzania Partnership imeshirikiana na Airtel toka mwaka 2012 katika kuhakikisha taarifa mbalimbali za kiafya zinawafikia watanzania bila gharama yoyote. Mpaka sasa mradi huu umekuwa na mchango mkubwa sana zaidi ya watumiaji laki 4 wameshajisaji na takribani meseji zaidi ya million 27 zenye taarifa mbalimbali za afya zimetumwa bila gharama yoyote. Tunawashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha mradi huu”.

“Taarifa tunazotuma kwa njia ya ujumbe mfupi ni pamoja na kumkumbusha mama mjamzito tarehe za kuhudhuria kliniki, Lishe bora, , maandalizi muhimu kabla ya kujifungua na kuwakumbusha kuhakikisha wanakwenda kujifungulia kwenye vituo vya afya vyenye wataalam wenye ujuzi. Napenda kuwaasa wakina mama kujisajili kwa kupitia simu zao binafsi au kusajiliwa na watoa huduma za afya pale wanapotembelea kliniki na hapohapo wataanza kupokea taarifa hizi muhimu buree bila gharama yoyote. Alisisitiza Saulo.

Kwa upande wake Mkazi wa Yombo na mfanyabiashara ndogondogo Bi Mwajuma Ally alisema “ huduma hii imekuwa muhimu sana kwangu kwani nimeweza kupata taarifa muhimu za afya ikiwemo dalili za hatari, muda wa kupumzika na kucheza kwa mtoto tumboni , elimu ya kumnyonyesha mtoto na nyingine nyinge. Mpaka sasa nimeweza kuwaunganisha kina mama wenzagu wa 3 na napenda kutoa wito kwa wa kina mama wengine kujiunga kwenye huduma hii inayopatikana kupitia mtandao wa Airtel bila gharama yeyote. Kwa kweli tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha sisi wamama na watoto wadogo kuwa na afya bora wakati wote.”

Kwa upande wake Meneja Huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema “sisi kama wadau wa huduma za mawasiliano tunatambua jinsi mawasiliano yalivyo na mchango mkubwa katika jamii na tunajisikia furaha kuwa mtandao wa kwanza ulioondoa gharama kwa wateja zaidi ya milioni 10 kupata taarifa hizi za afya bure bila gharama yoyote. Lengo letu ni kuhakikisha tunatoa fursa mbalimbali kupitia huduma za mawasiliano na kuokoa vifo vya kinamama na watoto wachanga vinavyochangiwa na ukosefu wa elimu ya kutosha.”

Kutokana na mafanikio ya mpango huu sasa taarifa za afya kwa watoto hususani juu ya lishe bora na chanjo zimeoongeza wigo kwa watoto wa hadi miaka mitano tofauti ambapo ilikuwa hadi kwa watoto wa wiki 16. Hii itasaidia kupunguza tatizo la utapiamlo na magonja hatarishi yanayowakumba watoto katika umri mdogo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)