Pages

Vijana watakiwa kuleta maendeleo barani afrika

 Naibu Waziri wa Afya Wanawake Jinsia na Watoto , Dk Hamisi Kigangwala akifungua Kongamano la Vijana barani afrika juu ya Maendeleo barani Afrika.
 Washiriki wa Kongamano hilo Vijana kutoka nchi Mbalimbali  wakifatilia Hotuba ya Dk Kigwangala
Na Humphrey Shao

Vijana barani Afrika wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika  kueleta Maendeleo hili kufikia malengo hasa katika kipindi hiki cha mapinduzi ya Teknolijia na Viwanda.


Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya Wanawake Jinsia na Watoto, Dk .Hamisi


Kigwangalla alipokuwa akifungua kongamano la Vijana barani Afrika lililoandaliwa na Tasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es Salaam.


Akizungumza kwa Niaba ya Makamu wa Rais Kigwangala amesema kuwa mara zote vijana 

wanapokusanyika na kujadili maendeleo ya bara la Afrika ni muhimu sana kwani leo 
vijana ndio wadau wakubwa katika swala zima la maendeleo ya bara lao  .


“inaeleweka kabisa ukuaji wa bara la Afrika unategemea vijana ndio maana ajenda ya 2063


inahusisha ubunifu , Nishati , utamaduni na swala zima la siasa safi  kama serikali tunawahimiza vijana kujitambua na kuwawezesha  kufikia malengo hili kuweza kupambana na vikwazo vinavyo wakabili” amesema Kigwangala.


Ameongeza kuwa vijana wanatakiwa kutambua vikwazo vinavyo wakabili kama fursa ya kujipatia maendeleo kwa kutatua vikwazo hivyo kwa ajili ya maendeleo ya vijana wa kesho.


Amesema mjadala wa leo sio tu kwa ajili ya Vijana bali ni kwa ajili ya maendeleo ya bara la


Afrika kwa kuwa na sera zitakazowawezesha vijana.
 Rasi wa Vijana Barani Afrika , Francine Muyumba  akizungumza na Vijana mbalimbali kutoka nchi mbalimbali ambao walishiriki kongamno hilo la Vijana washiriki wa Kongamano wakisikilza kwa makini
 Mmoja wa Vijana kutoka nchini Nigeria, Arinze Obiezue  akitoa neno la shukrani kwa naiba ya washiriki wa kongamano hilo.
 Viongozi wa meza kuu wakiongoza na Naibu Waziri wa Afya , Dk Hasmisi Kigwangalla  wakisikila maneno ya shukrani kutoka kwa kijana
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri na Washiriki wa Kongamano hilo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)