Pages

SAMIA ATAKA KASI KUONGEZA UWEKEZAJI

MAKAMU wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuongeza kasi katika uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora nchini ili tufike tunakotaka yaani uchumi wa viwanda ifikapo 2025.
Akizungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Makamu wa Rais alisema kwamba serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na kwamba mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mengi yanatafutiwa ufumbuzi.
Alisema mwaka wa kwanza wa serikali ulikuwa ni wa kazi nyingi na hivyo serikali ilikuwa ikitafuta fedha na kwamba sasa wametulia na wataleta nafuu kwa mujibu wa sheria na matakwa ya sasa ya kukuza uchumi.
Alisema serikali ipo tayari kufanyakazi na wenye viwanda kwa sababu inaamini mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kuondoa umaskini, kukuza ajira na kuimarisha mwelekeo kwenda katika uchumi wa kati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipohutubia wakati wa hafla ya utoaji waTuzo za Rais za Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 zilizofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Thebeauty)
Makamu wa rais ambaye katika hotuba yake alikuwa anazungumzia changamoto zinazoikumba sekta binafsi katika kutekeleza wajibu wake, amesema kwamba serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto hizo na imechukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba zinamalizwa.
Hatua hizo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama bandari na reli na pia kuwapo kwa kamati inayoangalia kero zinazosumgua sekta ili serikali ifanye maamuzi.
Kwa sasa kuna kamati inayoangalia namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara inayofanyakazi  Wizara ya Viwanda na inakaribia kumaliza kazi yake na kuikabidhi serikalini.
Akizungumza kumkaribisha Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji ili amkaribishe Makamu wa Rais kuzungumza na washiriki katika hafla hiyo,Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Shabbir Zavery alitaja changamoto tisa zinazotia msukosuko ukuaji wa viwanda nchini.
Moja ya changamoto hizo ni mabadiliko ya mara kwa mara na ya ghafla ya sera au sheria za kibiashara ambayo huondoa utulivu kwa wazalishaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akirejea kwenye meza kuu baada ya kuhutubia wageni waalikwa kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Zavery alisema kwamba ufanisi na utuilivu wa kufanya biashara unategemea sana kutobadilika mara kwa mara kwa sheria na sera za biashara na mwaka uliopita serikali ilichukua maamuzi kadhaa bila kuhusisha sekta binafsi na hivyo kudhoofisha ushirikiano baina ya serikali na wafanyabiashara.
Pia alisema kwamba utitiri wa mamlaka za udhibiti na tozo zao mbalimbali pia kufanyakazi zinazofanana na kutembelea viwanda kwa kila mamlaka kwa wakati wake kunachangia gharama za kufanyabiashara.
Akizungumzia tatizo sugu la wenye viwanda na wafanyabiashara kutorejeshewa malipo stahiki (Vat na nyinginezo) wanazodai kutoka Mamlaka ya Kodi, na kodi zinazoua ushindani,Makamu wa Rais Samia amesema kwamba serikali kwa sasa imeshatulia na kwamba itaendelea kufanya marejesho kwa mujibu wa sheria na suala la kodi limeshafanyiwa maelekezo na kwamba wahusika wanatakiwa kukutana kushughulikia tatizo hilo.
Aidha ameiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuhakikisha kwamba utekelezaji wa mikakati ya kupunguza kero kwa wawekezaji na wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.
“Nafahamu kuwa sekta ya viwanda imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali. Serikali tunaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha viwanda vyetu vinakuwa katika mazingira rafiki na wezeshi ili kuwaongezea ufanisi na ushindani katika masoko ya kimataifa” alifafanua Makamu wa Rais.
Makamu wa pili wa Mwenyekiti wa CTI, Shabbir Zavery akisoma risala ya Mwenyekiti wa CTI kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais alikumbushia maneno aliyotoa katika ziara zake mikoani kwa taasisi za serikali na sekta binafsi kukaa, kujadili na kuona namna ya kuondoa adha katika uwekezaji na ufanyaji biashara bila kuipotezea mapato serikali.
Aidha alisema kwamba wakati serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuondoa changamoto zinazoathiri ukuaji wa sekta ya viwanda, ni muhimi pia kwa wawekezaji na wazalishaji kutambua majukumu yao katika kuchangia juhudi hizo.
Alisema majukumu hayo ni pamoja na kuzalisha bidhaa nyingi, zenye ubora na zenye bei rafiki kwa mlaji.
“Tusisahau kuwa sekta ya viwanda ina jumkumu kubwa sio tu la kuipatia serikali mapato; bali pia kutoa ajira kupunguza umaskini pamoja na kuijengea nchi heshima kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa kimataifa” alisema Makamu wa Rais.
Aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  kuratibu na kukutana na wizara au taasisi za serikali na za umma nchini ili kuwahamasisha kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kama ilivyoanza kwa vikosi vya usalama ambapo wanatakiwa kununua bidhaa zao hapa nchini.
Pia amewataka wafanyabiashara kuingia ubia na mifuko ya jamii ili kuwa na mitaji itakayowezesha kuanzisha viwanda kwa pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga alipokuwa akiwatambulisha wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan kuzungumza katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Nalo shirikisho hilo la viwanda limepongeza uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano kwa kufanya uwekezeji mkubwa katika sekta za kiuchumi zinazotengeneza njia kuelekea katika uchumi wa viwanda.
Wametaja uwekezaji huo kuwa katika umeme, barabara,reli, maji na bandari.
Katika risala ya CTI kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya utoaji Tuzo za Rais za Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016, wamesema uwekezaji huo utasaidia kushuka kwa gharama za uzalishaji na hivyo kuongeza ushindani  wa wazalishaji wa Tanzania katika soko la ndani na la nje.
Akisoma risala hiyo kwa Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa  Shabbir Zavery, alisema, pamoja na mafanikio katika miundombinu uwekezaji uliofanywa katika elimu utasaidia kutoa wataalamu wengi wenye tija katika sekta ya viwanda ambayo inategemea kukua kwa kasi katika kipindi kifupi kijacho.
Aidha alisema pamoja na changamoto zinazokabili sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji taifa katika awamu ya tano imeshuhudia kukua kwa pato la taifa kwa asilimia 6.75; kupungua kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 5.6 mwaka 2015 ukilinganisha na wastani wa asilimia 5.2 mwaka 2016.
Mafanikio mengine aliyoyaeleza Zavery ni kuongezeka kwa mauzo ya nje ambapo jumla ya dola za Marekani bilioni 9.38 zilipatikana ukilinganisha na dola za Kimarekani bilioni 8.92 zilizopatikana mwaka 2015.Likiwa ni ongezeko la asilimia 5.2.
Aidha katika Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mazingira Bora ya Biashara ya mwaka 2016 Tanzania ilishika nafasi ya 139 ikilinganishwa na nafasi ya 140 mwaka 2015.
“Vile vile usimamizi mzuri wa mapato ya serikali umewezesha kuongezeka mapato ya serikali kila mwezi kufikia zaidi ya shilingi trilioni moja ikilinganishwa na shilingi bilioni 900 zilizokusanywa mwaka 2015” alisema.
Alisema hata hivyo pamoja na mafanikio hayo ambayo yamepatikana katika kipindi kifupi, kuna changamoto ambazo kwa kiasi zinapunguza kasi ya mafanikio.
Mkurugenzi wa Ishara Consultants Ltd, Isaac Saburi, akitoa maelezo mafupi ya vigezo vilivyotumika kuwapata washindi wa Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na mazingira yasiyo rafiki kwa kufanyabiashara yanayochangiwa na  mabadiliko ya ghafla katika sera na sheria zinazohusiana na biashara.
Changamoto nyingine ni utitiri wa kodi na tozo , kutorejeshewa malipo stahiki ya kodi ya ongezeko la thamani,ushindani unaozuiwa na kodi ya VAT kwa mali ghafi, upungufu wa makaa ya mawe,vibali vya kazi na bomoa bomoa inayofanywa na  kampuni ya reli isiyofuata sheria.
Zavery aliomba serikali kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo ili azma ya kuwa na Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2020 inafanikiwa.
Katika juhudi za kuhakikisha kwamba kero zinashughulikiwa CTI imeandika waraka ambao umewasilishwa Wizara ya Viwanda ili kurahisisha ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Katika hafla hiyo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji , Mh. Charles Mwijage alisema kwamba wataendelea kushirikiana na CTI kuhakikisha kwamba vikwazo hivyo vinaondoka.
Alisema ipo mikakati ya kukabiliana na hali hiyo hasa utitiri wa mamlaka na kodi ili kuhakikisha kwamba viwanda vipya vinaongezeka na vile vilivyopo vinashamiri.
Alisema kwa mwaka 2015 hadi 2016 viwanda zaidi ya 2000 vimesajiliwa na mamlaka mbalimbali  ikiwamo EPZ, SIDO, NDC na TIC.
Amesema kwamba kwa sasa wizara yake imeweka mkakati mahsusi wa kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na katika hili wamepanga kukutana wafanyabiashara mjini Dodoma kutafakari changamoto mbalimbali.
Meza kuu ya kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo mshindi wa kwanza wa jumla alikuwa ni Tanzania Breweries Limited, akifuatiwa na Mufindi Paper Mills Company Limited na mshindi wa tatu alikuwa Kioo Limited.
Aidha kulikuwa na washindi katika viwanda vidogo vya kati na vikubwa.
Mshindi katika safu ya viwanda vidogo wa kwanza alikuwa Alliance Life Assurance Limited kwenye masuala ya fedha na bima na mshindi  mwingine alikuwa ni Prisons Corporation Sole katika biadhaa za ngozi na viatu.
Kwa viwanda vya kati katika hafla hiyo ambayo mdhamini wake mkuu ni Bank M, mshindi  katika ujenzi alikuwa Dharam Singh Hanspaul and Sons Limited; safu ya kemikali mshindi alikuwa Royal Soap and Detergent Industiries Limited; katika nishati ,umeme na elektroniks mshindi alikuwa Tanalec Limited na katika usindikaji wa chakula mshindi alikuwa Chemi Cotex industries limited.
Washindi wengine viwanda vya kati walikuwa Ital Shoe Limited katika bidhaa za ngozi na viatu; Chemi Cotex Industries limited katika bidhaa za metali ;Nyanza Mines (T) Limited katika bidhaa za madini; Hanspaul Automechs Limited safu ya magari na vifaa vyake; Tanpack Tissues limited bidhaa za karatasi na makasha na DPI Simba Limited katika safu ya bidhaa za plastiki.
Kwa viwanda vikubwa  washindi katika nafasi mbalimbali ni  Tanzania Breweries limited, Petrolube T limited, Petrofuel T Limited, Alliance Insurance Corporation Limited, Said Salim Bakhressa, Alaf Limited, Kioo Limited, Mufindi paper Mills Company Limited, Jambo Plastics na Nida Textile Mills T Limited.
Washindi wa tuzo hizo walipatikana kwa kuzingatia ufanisi katika uzalishaji, mauzo ya nje, uwekezaji katika teknolojia ya kisasa,matumizi bora ya nishati, utunzaji wa mazingira, afya na usalama wa wafanyakazi, uwiano wa kijinsia katika uongozi, pamoja na mchango katika jamii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi cheti kwa niaba ya ITV na RADIO One kwa kutambua mchangao wao wa kurusha LIVE matangazo ya hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimakbidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso cheti kwa kutambua mchango wao kwa kuwa mdhamini mkuu wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Jacqueline Mengi cheti kwa niaba ya magazeti ya The Guardian Limited kwa udhamini wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji Bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo hizo, Teddy Mapunda kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (wa tatu kulia) akiwa amejumuika na marafiki zake, Nancy Sumari Neghesti (kushoto), Nasreen Kareem (kulia) pamoja na Fausta Kameja (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali nchini waliohudhuria hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage walipowasili katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye wakielekea katika ukumbi wa Marquee kwenye hoteli ya Serena jana jijini Dar es Salaam ilipofanyika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vya umeme kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi alipotembelea banda la maonesho la Kilimanjaro Cables linalomilikiwa na kampuni hiyo wakati wa kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly ndani ya banda la kampuni hiyo maarufu kwa utengenezaji wa samani za ndani kwenye kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi akimsikiliza Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (aliyeketi) wakati akitoa maoni juu ya ubora wa samani hizo za ndani zinazotengenezwa na Kampuni ya Amorette Ltd inayomilikiwa na Bi. Jacqueline Mengi (hayupo pichani) katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga wakitia baraka kwenye banda la maonesho la Kampuni ya Amorette Ltd katika kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye banda la maonesho wakati hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Hanspaul, Kamaljit Singh Hanspaul (kushoto) kabla ya kuanza rasmi kwa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi (kulia) akifurahi jambo na rafiki yake Fausta Kameja katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, ambao ndio waratibu wa tuzo za CTI, Teddy Mapunda (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kushoto aliyesimama) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti mstaafu wa CTI, Dk. Reginald Mengi akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga (kulia) wakati wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji wa hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016, Bw. Innocent Mungy (wa pili kulia aliyesimama) akifafanua jambo kwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Serena.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank M, Jacqueline Woiso (kulia) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Viwanda, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Dk. Reginald Mengi mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akisamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi alipotembelea mabanda ya maonyesho katika hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Afisa Mauzo wa Kampuni ya Amorette Ltd. Brigitta Kelly (wa pili kushoto) alipotembelea banda ya kampuni hiyo inayojishughulisha na utengeneza wa samani za ndani (Furniture). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kammpuni ya Amorette Ltd, Jacqueline Mengi pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (aliyepo pembeni ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa AFRiCAB Group, Yusuf Ezzi (wa pili kushoto) alipotembelea banda Kilimanjaro Cables wauzaji wa vifaa vya umeme ambao walieleza wako mbioni kufungua kiwanda cha kutengeneza Transfoma za umeme nchini na kuongeza ajira. Kushoto ni Meneja Utawala wa kampuni ya AFRiCAB Group, Kunajal Gina na Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Rais za Wazalishaji Bora wa Viwanda kwa mwaka 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Bodi ya CTI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake walioshiriki kwenye hafla ya Tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora kwa mwaka 2016 iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)