Pages

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MTO RUAHA MKUU NA KUZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA IRINGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuangalia mto Ruaha Mkuu ambao kina cha maji kimeshuka sana kutokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimuelezea  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan namna mto Ruaha Mkuu ulivyoathirika kutokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu, Makamu wa Rais aliongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza kujionea madhara ya uharibifu wa mazingira kwenye mto Ruaha Mkuu.
 Kima cha Maji kikiwa chini kabisa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ambapo alimuelezea Makamu wa Rais kuwa Hifadhi hiyo inapata idadi ndogo ya watalii kutokana na barabara kutokuwa nzuri, gharama za usafiri wa anga kuwa kubwa ambapo Makamu wa Rais amemuahidi kulifanyika kazi suala la barabara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Iringa ambapo alisisitiza juu ya utunzaji wa Mazingira pamoja na kutunza amani ,kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa B. Amina Masenza akizungumza wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais na Wazee wa Iringa ambapo pia walialikwa viongozi wa dini, wakina mama, wafanya biashara na wanafunzi wa vyuo vikuu.
 Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Donald Mtetemela akizungumza wakati wa mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Iringa ambapo aliwataka wananchi wa mkoa huo kutunza mazingira hasa ya Milima ya asili ya mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mstaafu Abbas Kandoro akizungumza wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Wazee wa mkoa Iringa ambapo alihimiza Wazee wa mkoa huo kuungana katika kampeni ya kutunza mazingira.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)