Pages

KAMPUNI YA AGGREY&CLIFFORD YANG'ARA KIMATAIFA

 *Yatambulishwa kwenye orodha ya makampuni bora ya matangazo duniani 2017

Taasisi ya kimataifa ya masuala yanayohusiana na makampuni ya matangazo duniani ya thenetworkone ya nchini Uingerezaimetoa jarida lake la “The World’s Leading Independent Agencies”la mwaka 2017 mwishoni mwa wiki hiiambapo kampuni ya matangazo ya biashara na ushauri wa masoko nchini Tanzania ya Aggrey&Clifford, imetangazwa katika orodha ya makampuni bora duniani kutokana na mchango mkubwa inaotoa kukuza sekta hiyo.

Aggrey&Clifford, imechomoza miongoni mwa makampuni 12 duniani, matatupekee ndiyo yakitokea barani Afrika,yanayotoa mchango mkubwa katika kukuza sekta ya matangazo ya kibiashara na makala yake kuhusiana na umuhimu wa makampuni ya biashara kufanya ubunifu wa chapa zake za biashara,kuzilinda na kuziendeleza imechapishwa kwenye jarida hilo ambalo limeanza kuuzwa nchini Ungereza na pia likipatikana kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya leadingindependents.com.

Makala hiyo imeeleza kwa kina jinsi makampuni mengi yanayowekeza biashara zake barani Afrika yamekuwa na mtindo wa kunakili chapa za mataifa ya nje ya Afrika na mara nyingi kutumia matangazo ya biashara yaliyotengenezwa kwenye nchi hizo ambayo hayaendi sambamba na mazingira na masoko ya bara la Afrika.
Kupitia makala hiyo makampuni ya biashara barani Afrika yanashauriwa kuhakikisha yanafanya utafiti wa masoko na kuyaelewa vizuri badala ya kutumia chapa na matangazo yaliyotengenezwa kwa kulenga masoko ya sehemu nyingine.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Aggrey&Clifford, Rashid Tenga, akiongea kuhusu mafanikio haya alisema “Tunajivunia kuona kampuni yetu inafanya vizuri nje ya mipaka ya bara la Afrika katika ngazi ya kidunia, kwa kuingia katika World’s Leading Independent Agencies na ni moja ya hatua ya mafanikio katika kipindi cha miaka 8 tangia kampuni ianzishwe. Hatua hii inadhihirisha kuwa makampuni ya kitanzania na Afrika yanayo fursa ya kufanya vizuri katika ngazi ya kimataifa kama ambavyo imetokea.”

Tenga alisema Aggrey&Clifford, ambayo inafanya kazi na makampuni makubwa nchini na ukanda wa Afrika Mashariki, itaendelea kutoa huduma bora za matangazo ya biashara na ukuzaji wa chapa za biashara za kitanzania na kutoa ushauri.

Aggrey&Clifford yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam ikiwa na matawi katika nchi za Uganda (Kampala) na Rwanda (Kigali), mbali na huduma za matangazo ya biashara na ukuzaji chapa inatoa huduma mbalimbali za ushauri na ukuzaji wa huduma za makampuni ya biashara na Mashirika yasio ya kibiashara.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)