Pages

Hizi ndio sababu ya viwanja kupanda bei

Kiwanja hiki kinauzwa Kipo Kigamboni Kibada na kina ukubwa wa mita za mraba 1088 na kimepimwa na hati kinacho.

Kila kitu katika maisha kina thamani yake japokuwa vingine vimekuwa na thamani kwa muda mfupi tu lakini kadri muda unavyokwenda mbele ndivyo vinavyopoteza thamani lakini hali imekuwa tofauti kwa kitu kinachoitwa ardhi.

Ardhi imekua kitu ambacho kinapanda thamani mara kwa mara kutokana na jinsi maeneo husika yanavyozidi kukua na kuboreka na ndio maana waswahili wakaleta msemo wao kuwa ardhi ni utajiri.
Leo tutaangaza vitu vinavyoipandisha thamani ardhi. Ardhi imekua tunu sehemu yoyote pale duniani na ndio kitu ambacho ni gharama sana kukipata. Leo hii utakaponunua kipande cha ardhi kwa angalau shilingi za kitanzania Milioni 2 basi sehemu hiyo hiyo baada ya Miaka mitatu na kuendelea hapatauzwa shilingi milioni mbili tena bei yake itakuwa ya juu kutokana na thamani yake kupanda kutokana na vitu mbalimbali ambavyo tutaviona hapa chini. Basi ungana nasi kufahamu ni vitu gani vinaweza kupandisha thamani ya ardhi.

1:Miundombinu ya Barabara. Barabara ni nyenzo muhimu sana katika maisha ya binadamu. Barabara ni njia moja wapo ya mawasiliano katika ya kijiji na kijiji au mji na mji au nchi na nchi, sehemu inayokuwa na miundombinu ya barabara ambayo inapitika mwaka mzima iwe jua iwe mvua basi sehemu hio ardhi yake huwa na thamani zaidi kuliko sehemu ambayo kuna miundombinu mibovu ya barabara kama ilivyo hulka kwa binadamu kupenda vizuri basi binadamu tunapenda sana kukaa sehemu yenye barabara nzuri ambapo hata mvua ikinyesha kiasi gani hakutakuwa na adha ya usafiri na kusababisha kadhia katika watu kwenda kwenye mihangaiko yao. Kwa hiyo barabara ni nyenzo mmoja muhimu sana ambayo inafanya ardhi kupanda thamani.

2:Makazi ya Watu. Sehemu yoyote ile ambayo imeanza kujengeka basi ni dhahiri kabisa sehemu inapendwa na wengi kutokana na kuwa binadamu hawapendi kuishi peke yao kwasababu lolote linaloweza kutokea basi atapata msaada wa haraka kutoka kwa majirani. Sehemu yoyote iliyoanza kujengeka tunarajia kukuta kuona miundombinu kama maji, barabara, hospitali, shule, maduka  nk vinaanza kujengwa au kuwepo kwa uchache wake na pindi vitu hivi vinapoanza kupatikana kwa wingi maeneo hayo basi thamani ya ardhi kwa kipindi hiko hupanda tofauti na eneo hilo kabla halijawa na vitu hivyo.

3: Miundombinu ya Mawasiliano. Hakuna ambae hapendi kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki popote pale duniani. Na ndio moja ya nyenzo muhimu ambayo huleta watu karibu na kukuza uchumi. Sehemu ambayo hakuna miundombinu mizuri ya mawasiliano watu wengi hawapendi kuishi sehemu hizo. Ndio maana watu hupenda kusubiri sehemu hadi ichangamke ndio waweze kununa ardhi maeneo hayo na ndipo wanakutana na bei kubwa ya ardhi ukilinganisha na eneo lenyewe. Leo hii ukitaka kununua ardhi kariakoo unaweza usipate na hata kama utapata basi ni kwa bei ambayo wengi hatuwezi kuimudu yote hii ni kutokana na kuwa eneo hilo tayari lishachangamka na kuwa na miundombinu yote muhimu inayohitajika na binadamu. Kama unaweza kununua eneo leo hii sehemu ambayo wengi wanapaita porini basi utaweza kununua kwa bei rahisi sana kuliko eneo hilo likishachangamka.

4:Huduma za Kijamii. Hospitali, shule, viwanja vya michezo nk, hivi vyote vimekuwa sehemu ya kukuza thamani ya ardhi katika maeneo mengi na watu wengi wanapenda kuishi karibu na huduma hizi za kijamii ili kwao iwe rahisi sana kupata msaada pale wanapohitaji huduma flani. Ndio maana leo hii sehemu ambayo kuna hospitali kubwa, viwanja vikubwa vya michezo ni dhahiri kabisa maeneo hayo thamani ya ardhi itakuwa juu kulinganisha na maeneo ambayo hakuna vitu hivyo.

5: Usalama. Usalama ndio silaha kubwa kwa binadamu yoyote Yule. Hakuna binadamu asiyependa kuishi kwa amani na usalama. Sehemu yoyote yenye usalama ndio sehemu ambayo watu wengi wanapenda kuishi kutokana na kwamba roho zao hazitakuwa juu juu bali watakuwa na utulivu wa hali ya juu sana. Ndio maana katika maeneo mengi yenye viashiria vya wizi na ujambazi wa kupindukia sehemu hizo zimekuwa zinasumbua sana watu kuishi na kufikia hatua ya watu kutaka kuhama na wengi kuuza maeneo yao kutokana na hali ya vitisho kama hivyo ambavyo huwafanya  roho za watu ziwe juu juu, maeneo kama hayo ambayo hayana usalama bei ya ardhi inaweza kuwa ni nafuu sana kutokana na mahitaji ya watu kuwa wachache japokuwa sehemu nyingine ambazo hazina usalama wa kutosha bado gharama za ardhi ni kubwa sana hii kutokana na vitu vingine ambavyo hupandisha thamani ya ardhi kuwepo maeneo hayo.

Kwanini vitu hivi hufanya ardhi kupanda thamani yote ni kutokana na sehemu husika kuwa na maendeleo, kila binadamu anapenda maendeleo na ndio maana sehemu yoyote ile iliyopiga hatua katika kuwa na miundombinu ya barabara, huduma za kijamii, miundombinu ya mawasiliano na vingine basi maeneo hayo huwa yamechangamka kutokana na watu wengi kujenga na kuweza kuishi maeneo hayo.

Ushauri wa bure ni pale ambapo kama unaweza kununua ardhi leo sehemu ambayo leo hii panaitwa porini basi nakushauri ukanunue sasa hivi kwa maana maeneo yote unayoyaona leo mjini yalikua kama hapo ila kutokana na mji kukua na maingiliano ya watu, ujenzi ndio yanafanya eneo husika kuwa na maendeleo sehemu ambapo hakuna binadamu basi sehemu hiyo inakuwa haina maendeleo mazuri kwasababu hakuna anayeishi .

Na hizi ndio sababu kwa nini leo hii usinunue kiwanja hiko kinachoonekana pichani ambacho kipo Kigamboni Kibada , Eneo kilipo kiwanja hiki tayari kuna miundombinu yote muhimu japokuwa ndio pameanza kukua kutokana na watu kuanza kujenga  makazi yao maeneo haya ya Kibada. Ni sehemu ambayo bado haijawa na muingiliano mkubwa wa watu na kusababisha usalama kuwa mkubwa  sana

Kwanza hali ya hewa ya Maeneo ya Kibada ni nzuri kupita maelezo kutokana na kuwa karibu na pembezoni mwa bahari ya hindi kitu ambacho hufanya maeneo haya kuwa na hali nzuri ya hewa kama vile baridi kiasi huku joto likiwa la msimu. Vile vile ununuapo kiwanja hiki basi fahamu kuwa gharama ya ujenzi kwako itapungua kutokana na kwamba upatikanaji wa mchanga hautokusumbua kwasababu mchanga unapatikana hapo hapo katika kiwanja chako ambacho wewe utachimba pindi uanzapo ujenzi wa makazi yako. Maji pia yapo Ni kiasi cha wewe tu kuamua.


Ukubwa wa kiwanja hiki ni mita za mraba 1088 huku kikiwa kimepimwa na kupewa hati na pia kipo mbele ya barabara kuu ya mtaa ambayo inaelekea barabara kuu ya kigamboni ferry au kongowe lakini Pia ni mita chache kutoka barabara kuu ya kigamboni . Pamoja na yote ni sehemu ambayo ina mpangilio mzuri wa ujenzi wa makazi ya watu huku huduma zote muhimu zikipatikana kama vile maji, hospitali ya Kibada, Shule ya msingi na awali nk. Lakini sehemu hiyo kwa mbeleni kutakuwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi maana tayari alama zishawekwa kuhamisha watu waliopembezoni mwa hifadhi ya barabara. Bei ya kiwanja hicho pichani kwa sasa ni nafuu kuliko utakapotaka kununua kipindi eneo hilo limechangamka na kuwa na maendeleo zaidi ya yaliyopo leo hii. Na kama utakuwa unahitaji kununua kiwanja hiki basi unaweza kuwasiliana na Muhusika kwa namba hii 0786 821 613

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)