Pages

Droo ya Milioni 10 ya nguvu ya buku kuchezeshwa Jumapili hii

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHEZO wa bahati nasibu unaoendeshwa na Biko, unaotambulika kama Ijue nguvu ya Buku unatarajiwa kuchezesha droo yake ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, Jumapili hii.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James
Mbalwe (wapili kushoto), akimkabidhi Leseni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya BIKO Charles Mgeta kwa ajili ya kufanya shughuli za mchezo wa
kubahatisha nchini. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Kushoto
ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja
Masoko wa BIKO Goodhop Heaven. Picha zote na Mpigapicha Wetu.


Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James
Mbalwe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta mara baada ya kupeana leseni ya kufanya shughuli za mchezo wa


kubahatisha nchini unaoitwa kama Nguvu ya Buku. Hafla hiyo ilifanyika
Dar es Salaam jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biko, Charles Mgeta, alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu Mgeta, alisema droo yao itakuwa ya kwanza tangu walipoanzisha mchezo huo wenye zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10000, 20000, 50,000, 200,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya Sh Milioni 10 ikipatikana kila mwisho wa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea leseni ya uendeshaji wa michezo ya kubahatisha kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe wa pili kushoto. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven.

Charles Mgeta akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari juu ya kampuni yao ya Biko kuendesha michezo ya kubahatisha, ambapo Jumapili hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo baada ya kuipa leseni kampuni ya Biko inayondesha mchezo wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Biko, Goodhope Heaven, kulia akizungumza na waandishi juu ya mchezo wao wa kubahatisha unaojulikana kama Nguvu ya Buku, ambapo mwishoni mwa wiki hii watachezesha droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10.

“Leo pamoja na kutangaza juu ya kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 Jumapili, bali pia tumekabidhiwa rasmi cheti cha utendaji wa kazi zetu kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ambapo tunaamini safari yetu itakuwa ya mafanikio zaidi kwa Watanzania.

“Taratibu zetu ni rahisi kwa sababu washiriki wetu wanatakiwa kufanya miamala ya simu za MPESA, TIGO PESA na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni yetu ambayo ni 505050, huku pia akipaswa kuingiza namba ya kumbukumbuku ambayo ni 2456 ambapo kila ujumbe mmoja wa simu atatozwa kwa sh 1000, huku kiasi hicho cha pesa kikiwa na nafasi mbili ikiwa ni zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kumuingiza kwenye droo ya wiki ya kujishindia Sh Milioni 10,” Alisema.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, James Mbalwe, aliwapongeza BIKO kwa kuingia katika mchezo huo kama sehemu ya kuwapatia maisha bora Watanzania kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.

“Naomba kuwatangazia Watanzania kwamba BIKO wamesajiliwa rasmi katika kuchezesha michezo hii na tunawaambia kwamba wapo salama hivyo kila Mtanzania apaswa kucheza ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi wa zawadi mbalimbali,” Alisema Mbalwe.

Biko wameanza kuchezesha mchezo huo wa bahati nasibu huku wakiwa wamejiwekea malengo makubwa ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anajiwekea fursa ya kuibuka na ushindi wa zawadi mbalimbali kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha kutoka kwenye kampuni yao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)