Pages

Airtel yazindua duka la kisasa Babati Mkoani Manyara

Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara Peter Kimaro akitoa maelezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,  Francis Massawe kabla ya kukata utepe kuzindua duka jipya la Airtel lilopo Babati Mjini Mkoani Manyara
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,  Francis Massawe akikata utepe kuashiria ufunguzi wa  duka la  Airtel mkoa wa Manyara. wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,  Francis Massawe akiongea mara baada ya kuzindua duka la Airtel Mkoani Manyara  akishuhudia Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara Peter Kimaro
 Afisa wa kitengo cha huduma kwa wateja wa dula la Airtel Manyara  Bi Ramla Rajabu akimuonyesha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,  Francis Massawe  baadhi ya simu zinazopatikana katika duka jipya lililopo Babati mjini mara baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo jipya litakalotoa huduma kwa wateja na wakazi wa mkoa wa Manyara

Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imezindua duka mjini Babati kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wanaoishi katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Manyara ikiwa ni mwendelezo wa mpango wake wa kufungua maduka ya kutoa huduma kwa wateja wake nchi nzima.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara,Fransic Masawe,ndiye aliyezindua duka hilo ambaye amesema litasadiai kutoa huduma kwa wakati lakini pia lisaidia kutoa ajira kwa vijana na kuwawezesha wakulima wa mazao ya  kupata huduma za kifedha kwa urahisi zaidi

 “ nawapongeza Airtel kwa kusogeza huduma karibu na wateja  na kuongeza kuwa duka hilo litakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mji wa Babati  pamoja na maeneo jirani. Napenda kuchukua fursa hii kuwa kuwaasa wakazi wa hapa hususani vijana kuchangamkia fursa za ajira zilizopo kupitia duka hilo ajira kwa lengo lakujiongezea kipato”. Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Fransic Masawe

 Kwa Upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara,Peter Kimaro,amesema duka hilo linalenga kusogeza huduma karibu na jamii kwani kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanapata tabu kupata huduma za uhakika lakini pia hatua hiyo inatoa mwanya wakuongeza maduka mengine mengi katika maeneo ya mkoa huo ikiwemo wilaya  ya Katesh

Pia amesema huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo kwani inasaidia uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kuwawezesha huduma za kifedha kupatikana kirahisi ambapo kwa sasa watu wengi hutumia Airtel Money kufanya miamala pamoja na kupata mikopo kupitia huduma ya Airtel Timiza ambayo imekuwa ni mkombozi kwa wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji ya kuendesha biashara zao.

Tunatoa wito kwa wateja wetu kutembelea maduka haya ambayo tunayafungua nchi nzima ili kupata huduma hapa manyara tayari tunayo maduka matatu ambayo moja tunalizindua hapa na mengine mawili yapo katika maeno ya Dareda center na Riloda .aliongeza Kimaro


Baadhi ya wananchi wamesema kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza ajira kwa vijana pamoja na kutoa huduma za uhakika za miamala ya fedha na mawasiliano kwa ujumla tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa wanalazimika kufuata huduma umbali mrefu kidogo

Kampuni ya Airtel inampango wakuongeza maduka mengine katika mkoa huo wa Manyara ili kuendelea kusogeza huduma zake kwa wateja kwa urahisi hususani katika maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)