Pages

VANESSA MDEE, DUMISHA HERI WAENDELEA KUSOTA RUMANDE KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watuhumiwa wawili  wanaodaiwa kujihusisha usambazaji wa dawa kulevya pamoja na utumiaji wa dawa hizo.

Watuhumiwa hao ni mwanamziki Vanessa Mdee na Dumisha Heri ambao wamekamtwa na polisi hivi karibuni.

Akizungumza  leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Polisi (CP), Simon Sirro amesema wasanii hao walikamatwa hivi karibuni katika mazingira ambayo hakutaja kutokana na masuala ya kiupelelezi.
Amesema kuwa baada ya kukamilika kwa  upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanaojihusisha na utapeli kwa kutumia vicoba kuhusisha majina ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP , Dk. Reginald  Mengi ,Mke wa Rais Mstaafu na Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Salma Kikwete pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

Amesema kuwa matapeli hao wametengeneza mtandao wa Focus Vicoba ambao watu wakiingia katika mtandao huo wanakuta taarifa mbalimbali zikiwemo za viongozi na watu wenye uwezo wa kifedha kuwa ndio wanaoendesha Vicoba hiyo kwa kutumia namba za simu za 0757 308381 na 0768 199359 ambazo sio namba za viongozi hao.

Kamishina Sirro amesema kuwa mwaka jana walimkamata Boniface Samson Ojwando (27) kwa tuhuma za kuhusika katika matandao huo na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kwa mtandao wa kijamii.

Kamanda Sirro amesema matapeli wengine walikuwa wanatumia gari  zenye namba usajili T 400 CNC aina ya Toyota  Mark II Grand  katika maeneo ya Sinza kwa madai kuwa linauzwa baada ya na baada kukubaliana maziano hufanya  uhalifu wa kupora fadha hiyo iliotaka kununulia gari hilo.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limekusanya zaidi ya milioni 840 za makosa mbalimbali ya usalama Barabarani.
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika operesheni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi leo jijini Dar es Salaan.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)