Pages

TANAPA YAWAPA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI NA UPIGAJI PICHA WAHIFADHI UJIRANI MWEMA NCHINI


Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) katika kuhakikisha kuwa linaboresha mawasiliano yake baina ya wananchi wanaoishi maeneo jirani na hifadhi wameamua kuwapa mafunzo maalum ya wiki moja yanayolenga kuwajengea uwezo Wahifadhi Ujirani Mwema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku hususan utoaji wa Elimu ya Uhifadhi kwa


wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi nchini.Miongoni mwa mammbo ambayo wameweza kujifunza ni utoaji taarifa kwa njia ya habari. Ilikufanikisha hilo TANAPA imewapa mafunzo ya kitaalam maofisa wake hao katika mafunzo yanayoendelea mjini Dodoma. Pichani juu ni Mhariri wa Habari Mwandamizi wa Machapisho ya Mwisho wa wiki ya Gazeti la Habarileo, kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Oscar Mbuza akitoa mafunzo ya uandishi bora wa habari za kijamii kwa maofisa hao.

 Maofisa Uhifadhi Ujirani mwema kutoka hifadhi mbalimbali nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo ya uandishi wa habari.
 Maranyingi habari huendana na picha, ili somo hilo la Habari liwezuri na liende sawa maofisa hao pia walipewa mafunzo ya namna ya upigaji picha bora za Habari na namna ya kutumia Kamera. Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti ya Serikali (TSN), Mroki Mroki alitoa mafunzo hayo kikamilifu.
 Muda wa majadiliano ulikuwepo baada ya kutoa mada, ambapo pia maswali yaliulizwa na kujibiwa.
 Washiriki wakifuatilia kwa umakini somo la upigaji picha.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi nae alishiriki mafunzo hayo kama mwenyekiti wa mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo. Source: TSN Digital

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)