Pages

Rais Magufuli amteua Bi. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,IKULU
01 Machi, 2017

Dar es Salaam

IMG_3758.JPG

Masahihisho toka Ikulu:

Mama Salma Kikwete ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na SIO Mbunge wa Viti Maalum kama ilivyoandikwa awali.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)