Pages

KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Baadhi ya maofisa wa TBA wakiwa kwenye mkutano na 
wajumbe wa kamati hiyo.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba Bunju B jijini Dar es Salaam jana. Wa nne kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.
 Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa katika mradi  wa Bunju B
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga, akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.
 Baadhi ya nyumba zinazojengwa kwenye mradi wa Bunju B
Mwonekano wa nyumba hizo.

Na Dotto Mwaibale

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuchangamkia nyumba zinazojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), ili kupata makazi bora baada ya kustaafu.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Josephat Asunga wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba inayofanywa na TBA jijini Dar es Salaam jana.

"Nawaomba watumishi wa umma kuzichangamkia nyumba hizi ambazo kwa  wao wanafursa ya kukopeshwa na kulipa deni polepole" alisema Asunga.

Alisema nyumba hizo zimejengwa na kuwekewa miundombinu mizuri hivyo kuwa ni sehemu bora ya kuishi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nyumba Tanzania (TBA), Mhandisi Elius Mwakalinga alisema nyumba zinazojengwa na TBA bei yake ni ndogo ukilinganisha na zile zinazojengwa na watu wengine.

"Hapa kwetu bei ya nyumba inaanzia sh.milioni 35 hadi milioni 200 wakati  maeneo mengine ni kuanzia sh.milioni 600" alisema Mwakalinga.

Alisema ujenzi wa nyumba hizo unakwenda sanjari na miundombinu yake na mahitaji mengine kama soko, bustani na  maegesho ya magari.

Alisema katika awamu ya tatu ya mradi TBA walipata mkopo wa sh.Bilioni 25 ambapo hadi Februari 2017 walipata mkopo wa sh.Bilioni 19.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuwauzia watumishi wa umma.

Alisema katika awamu ya pili ya mradi huo jumla ya nyumba 160 za aina tofauti zinaendelea kujengwa za zipo katika hatua mbalimbali, ambapo nyumba 64 zipo kwenye hatua za mwisho tayari kwa kuuzwa na nyumba 96 bado zipo kwenye hatua ya msingi na zilitarajiwa kujengwa kwa kutumia mfumo wa "Lunnel Forwork System"

Akizungumzia changamoto katika mradi huo alisema watu kujenga nyumba katika baadhi ya viwanja ndani ya eneo la mradi hivyo kupunguza idadi ya nyumba zilizokusudiwa kujengwa katika hatua za awali za awamu ya tatu ya mradi.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni kupatikana kwa malighafi mbalimbali za ujenzi hasa mawe, nondo hivyo kupunguza kasi ya ujenzi, upungufu wa fedha za utekelezaji wa mradi, kupanda kwa gharama za ujenzi kutokana na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi.

Alisema ili kupunguza gharama za kununua vifaa vya ujenzi  wakala amekuwa akienda kuvinunua moja kwa moja kiwandani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)