Pages

Airtel yazindua mnara mpya wa mawasiliano kata ya Mponde Tanga

Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo  wa Airtel Tanga John Nada wakikata autepe kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.

Airtel yapeleka mawasiliano kwa vijiji 16 mkoani Tanga
mnara mpya wa airtel kata ta Mponde wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Mawasiliano mapya vijiji 16 kuimarisha ulinzi na mawasiliano kwa jamii.
Tanga  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewafaidisha zaidi ya wakazi elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na mfuko wa Maendeleo wa mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication Services Fund.
Uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel katika kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga, umekuja ikiwa ni wiki moja toka Mfuko wa maendeleo wa Mawasiliano kwa wote na Airtel walipozindua minara mingine mitatu mkoani Dodoma.
akiongea wakati kuzindua mnara huo Meneja Mauzo wa Airtel Tanga  John Nada alisema  "Airtel tumejipanga kuendelea kutoa mawasiliano ya uhakika hasa kwa kipindi hiki ambacho TCRA wamezindua huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa na namba ileile ikiwa hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa wakazi wa Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre  Airtel ndio mtandao wenu wa ukahika kwa sasa”
“tunawaomba wakazi wote mtumie fursa hii ya mawasiliano kwa kuwa wabunifu zaidi,  tumumieni huduma ya Airtel Money kwa kuwa pia mko mbali na huduma za kibenki tumeni na kupokea pesa ili kuboreshe kilimo kwa kutumia mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel” alisisitiza Bw, Nada
Kauli ya wananchi  juu ya tatizo la mawasiliano zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda kwamba wakazi wa  Kata hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na kwenye vilele vya milima wakitafuta mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya kibiashara na mambo mengine ya kijamii.
“Tunawashukuru sana Airtel na UCSAF kwa jitihada zao za kutuletea mawasiliano, mawasiliano haya yatasaidia wakazi wa hapa kijijini na pia yatawasaidia wanaishio mbali na hapa ili kuweza kufanya shughuli zao vyema, awali hali ilikuwa mbaya sana, ilikuwa huwezi kupiga simu mpaka ufike sehemu yenye muinuko” alieleza Mh Mahunda-Diwani
Diwani huyo aliendelea kusema kuwa “ninawaahidi wadau wa mawasiliano Airtel na UCSAF kwamba tutayalinda mawailiano haya na tutayatumia vyema ili kukuza shughuli za maendeleo ya kijamii na uchumi wa Wilaya yetu ya Bumbuli Mkoani Tanga

Pamoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimila na serikali pia Uzindunzi wa mnara huo katika kijijii cha kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga ilipambwa na ngoma na burudani za asili za vijiji hivyo ambazo huchezwa mara kwa mara wanapokuwa na jambo la furaha kwa jamii zao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)