Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akikata utepe wakati wa kuzindua moja kati ya maduka madogo madogo ya Airtel mkoani shinyanga ambapo jumla ya maduka 8 yazinduliwa katika mkoa wa Shinyanga. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bwn Sunil Collaso akifatiwa na Meneja wa Kanda ya kati wa Airtel , Bwn Stephen Akyoo
· Wateja wa Airtel kupata huduma kwa haraka na karibu zaidi
· Mradi huu utachochea upatikanaji wa huduma za kifedha
· Airtel yaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuendelea kuwekeza nchini
Shinyanga, Jumapili 18 March 2017, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kuzindua ma duka Saidi ya 2000 nchini utakaowawezesha wateja wake kupata huduma na bidhaa zake za kibunifu kwa urahisi zaidi
maduka haya ya Airtel yatakuwa na muonekano unaofanana na yatakuwa katika maeneo maalumu ambayo yatawawezesha maelfu ya wakazi kupata huduma kirahisi na kukidhi mahitaji yao kwa ufanisi zaidi
Maduka hayo yatatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kifedha, huduma za intaneti, kuongeza salio , kusajili namba na pia kuunganisha wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel
Katika kutekeleza mpango huo wa Airtel imezindua maduka 8 katika mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi uliofanywa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel ambapo Airtel imeeleza mpango wake wa kujitanua zaidi na ili kufikisha huduma zake karibu na watanzania waishio mjini na pembezoni ya nchi
Akiongea wakati wa uzinduzi maduka hayo mkoani Shinyanga, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso alisema” tunajisikia fahari kutangaza azma yetu kubwa itakayowezesha upatikanaji wa bidhaa na huduma zetu kirahisi zaidi na kuendelea kuthibitisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu huduma bora. leo tunazindua maduka 8 hapa shinyanga na mpango wetu ni kuwa na jumla ya maduka yapatayo 76 mkoani hapa
Tunaamini hii ni njia pekee ya kuwafikia wateja wetu kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati na vilevile kuwaunganisha na huduma na bidhaa zetu za kipekee na kibunifu zinazosaidia kutatua changamoto zao za kila siku za kijamii na kiuchumi. Mpango wetu ni kuwa na maduka kama haya takribani 2000 nchi nzima na tayari tumeshaanza kufungua maduka haya kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini. Aliongeza Colaso
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi Josephine Matiro alisema” Tunafurahi kuona juhudi zinazofanywa na Airtel katika kusogeza huduma zake na wateja wake lakini pia kutengeneza ajira kwa wengi. Tunaamini maduka yanayozinduliwa leo hapa Shinyanga na yale yatakayozinduliwa mbeleni yatachochea kwa kasi kwa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa urahisi na kwa usalama na kutoa mwanya kwa Maendeleo Mengi kuku a kiuchumi. Napenda kuwahamasisha wamiliki wa maduka kutumia fursa hii kutanua biashara zenu na kutengeneza ajira kwa vijana hapa mkoani Shinyanga.
Kuanzishwa kwa maduka haya sehemu mbalimbali nchini kunathibitisha kwa vitengo dhamira ya Airtel kuendelea kuwekeza nchini na Afrika kwa ujumla
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)