Pages

New Alert: Mkuu wa Mkoa Wa Dar ataja majina mengine 65 ya washukiwa wa Madawa ya Kulevya

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda.Picha na Maktaba.

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda muda mfupi uliopita ametaja majina mengine ya washukiwa wa madawa ya kulevya. Kabla ya Kutaja majina hayo Mkuu wa Mkoa wa Dsm amesema "Tuko na majina 65, nitahitaji kukutana nao ijumaa, wako wanaosemekana wanatumia, wako wanasemekana wanazo taarifa zitakazotusaidia"

Aliendelea kusema kuwa "Kuna ambao tuliwaita wako nje ya DSM, wapo waliotoa taarifa na watafika ila wapo waliokimbia tunawafuatilia na tutawapata wote"

Baadhi ya majina yaliyotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paul Makonda ni Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kinondoni kupitia CCM, Idd Azan, Mbunge wa Hai kupitia Chadema na Mkuu wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, na Mchungaji Gwajima. Wote hao wametakiwa kufika kituo cha polisi kati ijumaa saa tano kwaajili ya mahojiano.

Mara baada ya kutaja majina ya washukiwa wa madawa ya kulevya Mkuu wa mkoa aliweza kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari na kufanikiwa kujibu baadhi ya maswali huku mengine akisema kwa taarifa zaidi wakaulize kituo cha polisi kwasababu yeye akishawafikisha pale basi ni jukumu la polisi kuwafikisha mahakamani au kutowafikisha kutokana na kujiridhisha kwao.

Wakati akiendelea kuongea Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paul Makonda amesema Tumemaliza awamu ya kwanza ya vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi na akaendelea kusema Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana.

Mwisho Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda amesema anawashukuru watanzania walioko nchi mbalimbali kwa kunipigia simu na kunipa taarifa mbalimbali

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi..

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)