Pages

Msanii Wema Sepetu kujiunga na CHADEMA rasmi


CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya kikatiba namba 1 ya mwaka 2017 inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia waandishi wa habari na kuwakaribisha wanachama wapya waliojiunga leo akiwemo msanii Wema Sepetu.
a88bba6e-ed7e-422b-a17d-e0de0abb7490.jpg
Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile hati ya mashitaka iliyorekebishwa na kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu: Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura
fe6e1a3b-3fbd-4a15-ba8e-548f75c1b13b.jpgf182fb41-04e9-45df-a6be-0e48c1482adf.jpg
Baada ya hapa Mbowe ataongea na Waandishi.

Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa Wema na wenzake wawili akiwamo mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi. Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi Machi 15.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)