Pages

Mafunzo ya TPSF yawafikia wajasiriamali wa Dodoma

 Mkuu wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,Bi.Vumulia Nyamonga,akifungua mafunzo ya TPSF mkoani Dodoma
Mwezeshaji kutoka taasisi ya TPSF Celestine Mkama akitoa mada kwenye mafunzo  hayo
 Mmoja wa wawezeshaji ,Iringo Ringo akitoa mada kwenye mafunzo hayo
 Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya TPSF,Bw.Godfrey Sembeye,akiongea wakati wa mafunzo ya wajasiriamali mkoani Dodoma
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji

Mkuu wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,Bi.Vumulia Nyamonga,amewataka wajasiriamali kutumia elimu ya ujasiriamali inayotolewa na taasisi ya TPSF kuboresha biashara zao.
 
Akifungua mafunzo kwa wajasiriamali wa mkoani Dodoma yaliyofanyika katika ukumbi wa KKKT mkoani humo,Nyamonga ,alisema kuwa matokeo ya kupata elimu ni kubadilika hivyo anaamini elimu ya ujasiriamali watakayoipata itasaidia kuleta tija kwenye biashara zao.
 
“Nawapongeza TPSF kwa kazi nzuri mnayofanya kuhakikisha wajasiriamali wanapata ujuzi unaosaidia kuboresha biashara zao kwa kuziendesha kitaalamu  ili ziwe endelevu na natoa wito kwa wajasiriamali mnaobahatika kuhudhuria kwenye mafunzo haya kuwauliza masuala mbalimbali wataalamu yanayohusiana na changamoto mnazokumbana nazo  katika biashara ili wataalamu wawasaidie”
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya TPSF,Bw.Godfrey Sembeye,alisema kuwa taasisi yake imejikita zaidi kusaidia kukuza wajasiriamali wadogo kwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha ukuaji wa uchumi hapa nchini hivyo wanatakiwa kusaidiwa ili kuendelea kuchangia pato hilo.
 
Simbeye alisema takwimu zinazonyesha kuwa kundi hilo la Wajasiriamali ni zaidi ya milioni 3.1 hivyo wanatakiwa kusaidiwa ili kuendelea kuchangia pato la Taifa.
 
 Alisema kubwa lengo la mafunzo hayo kwa wajasiliamali ni kuwajengea uwezo katika biashara zao ili kuweza kujiendeleza zaidi na kuwasaidia kuongeza mitaji  na kuwatafutia masoko ya biashaara zao .
 
Simbeye alisema taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu ya mafuzo  kwa Wajasiliamali kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo njia ya redio,luninga,magazeti na tovuti ya taasisi hiyo.
 

Alisema mpaka saa elimu hiyo imeishawapatia mafunzo wajasiriamali waliopo katika mikoa ya Geita,Mbeya,Kigoma na Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)