Pages

Konyagi inaunga mkono upigwaji marufuku vifungashio vya Plastiki

 Kaimu Meneja Mkuu wa TDL,Devis Deogratius katika mahojiano na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam,(katikati) ni Afisa Mwandamizi wa Masoko wa kampuni hiyo,George Kavishe

Mfano wa chupa za kisasa zitakazotumika kufungashia bidhaa za TDL ambazo kwa sasa zinapatikana katika mifuko ya Plastiki

 Serikali imepiga marufuku ufungaji pombe kwa kutumia mifuko ya plastiki,Kaimu Meneja wa kampuni ya TDL maarufu kama Konyagi iliyopo chini ya TBL Group,Devis Deogratius,anaeleza msimamo wa kampuni kuhusu  hiyo.

Kampuni ya TDL imepokea vipi uamuzu huo wa serikali?

TDL inaunga mkono jitihada za serikali kupiga marufuku ufungaji wa pombe kwa kutumia mifuko ya plastiki nchini na siku zote tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kupambana na matumizi ya vifungashio hivi.

Mnayo mikakati gani baada ya  hatua hii?

Changamoto za kutumia vifungashio hivi katika bidhaa zetu tulishaziona na tuko  katika mchakato wa kuacha  kuvitumia kufungia bidhaa na badala yake tutatumia vifungashio vya kisasa vilivyotengenezwa  kwa malighafi ya kioo.

Tunajipanga kuhakikisha bidhaa zetu zote ambazo zinapatikana sokoni zikiwa zimefungwa kwenye mifuko ya Plastiki kuhakikisha sasa zinapatikana katika vifungashio vya kioo vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa zaidi.

Suala la vijana wadogo kutumia vinywaji vyenye kilevi na vinavyopatikana kiurahisi na kwa gharama nafuu unaliongeleaje?

 TDL pia iko tayari kushirikiana na  wadau wengine kutafuta suluhisho la kukabiliana na changamoto hii.

kuna haja ya wadau mbalimbali nchini kushirikiana kuhakikisha sheria ya kununua na kutumia vinywaji vyenye kilevi kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18 inatekelezwa

 Ili sheria hii ifanye kazi wadau wote tunapaswa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuhakikisha kila mtu anayefikisha umri wa miaka 18 anapatiwa kitambulisho cha taifa ambacho mnunuzi wa vinywaji vyenye kilevi atakayetiliwa mashaka ya umri atapaswa akionyeshe kabla ya kuhudumiwa kwenye  sehemu zinazouzwa vinywaji vyenye kilevi.

Mnao mkakati gani kutekeleza  amri hii katika kipindi kifupi kilichotolewa?

 TDL itaomba kibali kutoka mamlaka husika cha kupata muda wa kutosha kuondoa bidhaa zake zilizofungwa kwa mifuko ya plastiki zilizopo kwenye masoko ambazo ni Konyagi, Zanzi Cream Liqueur na Valeur Superior Brandy.

Pia TDL imechukua hatua za kumaliza tatizo la bidhaa zake kuigwa na wajanja na kuziingiza kwenye masoko kwa kuwekeza kwenye teknolojia ya hali ya juu ya vifungashio ambavyo sio rahisi kuigizwa na matapeli wanaotengeneza bidhaa feki za makampuni na kuziingiza kwenye masoko.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)