Pages

Airtel na TFF Waomba wadau wa Soko kuwasapoti Serengeti Boys

Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando akiongea wakati wa kuwapongeza vijana wa Serengeti boys kwa kufuzu kuingia katika michuano ya AFCON na kuwaomba wadau kuwasapoti wachezaji ii kuendelea kufanya vizuri. Kushoto ni Raisi wa TFF , Jamal Malinzi  na Mwenyekiti wa Soka la vijana Tanzania, Ayoub Nyezi (kulia)

Kampuni ya simu ya Airtel sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Jamal Malinzi wamewataka wadau kujitokeza kuisapoti timu ya vijana ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys ambao wamefanikiwa kwenda kombe la Mataifa Afrika kwa vijana (AFCON) nchini Gabon mwezi Mei mwaka huu.

Malinzi alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupata nafasi ya ushiriki kwa vijana hao baada ya timu ya Congo Brazaville kushindwa kumpelekea mchezaji wao Langa ambae alisadikiwa kuwa na umri mkubwa zaidi na kuchezeshwa kwenye mashindano ya vijana.

Malinzi amewataka wadau kwa pamoja kusaidiana nao katika kuaindaa timu ya vijana kwani hakika mashindano haya yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha takribani dola laki tano (500,000) ili timu iweze kuweka kambi nje ya nchi na hata kupata vifaa vya kutosha na vya kisasa.

Meneja wa Mawasiliano  Airtel, Jackson Mmbando amesema kuwa wanawapongeza TFF kwa hatua kubwa waliyofikia ya kuifikisha hapa Serengeti Boys ila bado vijana hawa wanahitaji kupata sapoti kutoka kwa wadau na seriakali kwa ujumla.

Mmbando amesema kuwa,  vijana hawa wanahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi na kujengwa kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri kwani waliona walishaondolewa  kwenye michuano hiyo.

"Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili waweze kufanikisha safari yao ya Gabon mwezi wa tano na sisi kama airtel tutasaidia katika kuitangaza timu hiyo,"amesema Mmbando

Airtel wamekuwa wadau wakubwa sana wa kukuza soka la vijana kwa kuanzisha mashindano ya Airtel Rising Star ambapo hivi karibuni waliweza kufanya usaili wa vijana na wengine wakiwa tayari kwenye kikosi cha vijana wa Serengeti Boys.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)