Pages

Airtel money yaja na ofa kabambe

Meneja Uhusiano wa Airtel akitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote. Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na huduma nyingi zenye faida zaidi kwa kupiga tu *150*60#

Dar es Salaam Februari 2, 2017, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imezindua na  kuitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote.

Akiongea kuhusu Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando aliseme “Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na mambo lukuki ikiwemo

Kutuma pesa kwenda mitandoa yote kwa bei nafuu wateja wetu wanaweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa tozo ileile wakati wowote mahali popote pale nchini. Haya ni mapinduzi ya kipekee katika huduma za kifedha ambapo tumewezesha wateja wetu kufanya miamala hiyo kwa urahisi zaidi bila kujali gharama.

Kupata vifurushi  bora kupitia Airtel Money OFA KABAMBE vyenye ujazo zaidi kuliko vifurushi vya mitandao mingingine yote: Kupata hii piga *150*60# kisha nunua kifurushi kupia Airtel Money kwa kuchagua No.6 OFA KABAMBE , Pia vipo vifurushi vya UNI packs sasa vinapatikana kupitia huduma ya Airtel Money hivyo kuwawezesha wanafunzi kujiunga na vifurushi hivyo kwa urahisi zaidi

Kutuma pesa kwenda benki na kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Airtel Money kwenda Benki-  sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kufanya miamala hiyo kwenye benki 38 ambazo tayari tunaushirikiano nazo. Kadhalika wateja waweza kutumia ATM za umoja switch na CRBD zaidi ya 1105 nchini kwa kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money masaa 24 kila siku. ushirikiano huu umeongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi

Na pia tunawewezesha wateja wetu kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana  kwa wateja wetu na mawakala nchini, Mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi laki 5 na kujipangia yeye mweye alipe lini SIKU, WIKI au baada ya  MWEZI. Airtel Timiza ni suluhisho kwa mahitaji ya mikopo ya haraka ya kutatua changamoto za kijamii lakini pia inawawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji kwaajili ya biashara  zao papo hapo.

“Ndio maana tunaseme? Relax Airtel Money mambo yote” alisisitiza Mmbando

Huduma ya Airtel Money, kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi ya kifedha nchini hasa  katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za kibenki. Mwezi uliopita Airtel Money pia ilifanikiwa kugawa gawio la shilingi bilioni 3.5 kwa watejawake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)