Pages

TTCL yadhamini michuano ya vyuo Soka la Ufukweni


Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa tatu kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (wa tatu kulia) fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa nne kushoto) mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.


Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi (wa pili kushoto mbele) akizungumza kwa niamba ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba kwenye hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ufukwe wa Coco Beach na kushirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam wa Kampuni ya  TTCL, Jane Mwakalebela akiwa katika uzinduzihuo.


Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (katikati) akimkabidhi kiasi cha fedha shilingi laki nne (400,000/-) pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (5GB) kwa muda wa mwezi mmoja nahodha wa timu ya Chuo cha Ardhi (kulia) baada ya kuibuka washindi wa pili wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF). Mashindano hayo yalifanyika Ufukwe wa Coco Beach jana. Kulia ni Bw. Dimo Dibwe muandaaji wa mashindano hayo.


Baadhi ya waamuzi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakijadiliana jambo kabla ya mechi kuendelea.



Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.



Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.




Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.




Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.



Wakati mashindano hayo yakiendelea wanafunzi wa vyuo waliendelea kujishindia zawadi mbalimbali. Kushoto ni Ofisa Masoko wa TTCL, Eric Muganda akimkabidhi vocha ya muda wa maongezi wa thamani ya shs10,000/- baada kushinda moja ya michezo iliyoambatana na zawadi kwa wanafunzi waliokuwa wakishiriki mashindano ya soka la ufukweni. 




Baadhi ya timu zilizoshiriki Mashindano ya vyuo Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' zikishangilia baada ya kushinda mechi za awali.



Mbwembwe za mabingwa...! Mabingwa wa Mashindano ya Vyuo Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' wakiwa katika moja ya pozi mara baada ya kutangazwa kuwa mabingwa.


Kikosi cha Timu ya Chuo cha Ardhi ambao waliibuka washindi wa pili katika Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TTCL ambao ni wadhamini wa mashindano hayo.














KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imedhamini mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliozikutanisha timu za mchezo huo kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi kwa niamba ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba alisema kudhamini kwa mashindano hayo ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuiunga mkono Serikali kukuza michezo anuai nchini.

Alisema TTCL inatambua kuwa michezo inamanufaa makubwa kwa jamii hasa kundi la vijana kwani licha ya kuwakinga na baadhi ya magonjwa na kudumisha ushirikiano baina yao, pia ni sehemu ya ajira ambayo imekuwa ikiwapatia baadhi yao vipato halali na kuendesha maisha yao vizuri.

Alibainisha michezo ina faida nyingi ikiwemo kuwafanya washiriki kuwa watu wenye afya njema ya viungo mbalimbali vya mwili, afya ya akili na uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za maisha hivyo kujenga jamii ya watu wenye afya na furaha wakati wote jambo ambalo ni zuri kwa jamii nzima.

"...Kimsingi kwetu TTCL ni siku muhimu ambapo kwa mara nyingine, tunaungana na Wanamichezo kufanikisha tukio hili kwa udhamini wetu wenye nia ya kuithibitishia jamii kuwa kampuni ya TTCL ni mali yao, ipo kwa ajili yao na inatimiza kwa vitendo mpango wake wa kuipatia jamii huduma bora za Mawasiliano ya simu na intaneti zenye kiwango cha juu kabisa cha ubora na gharama nafuu.

"TTCL ni Wadau wakubwa wa sekta ya Michezo nchini. Wafanyakazi wa TTCL wanao utaratibu wa kushiriki michezo mbali mbali na mabonanza ya kila mara ili kujenga afya zao na kuongeza ushirikiano miongoni mwao. TTCL tunaamini kuwa, Michezo ni afya na kiungo muhimu cha mahusiano mema sehemu za kazi," alisema Mushi akimuwakilisha Kindamba katika uzinduzihuo.

Aidha aliongeza kuwa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, watoto na vijana wanaoshiriki katika michezo mbalimbali katika shule zao hujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, sigara na vitendo vya ngono ikilinganishwa na wale ambao hawajihusishi au kushiriki katika michezo, huku zikibaini wanafunzi wa kike wanaojihusisha na michezo katika ngazi mbali mbali za elimu kuwa na maendeleo mazuri ya kitaaluma jambo ambalo linapaswa kusisitizwa.

Alisema TTCL inaahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Vyama vya Michezo na Vikundi mbali mbali katika kuendeleza sekta ya michezo. Ametoa wito kwa Wanamichezo na Wananchi kwa ujumla kuiamini kampuni hiyo ya kizalendo na kuiunga mkono kwa kutumia huduma na bidhaa za TTCL.

"Nunueni laini za simu za TTCL, pigeni simu na kutuma ujumbe mfupi kupitia line hizi, nunueni vifurushi vya data vya TTCL ili muweze kuperuzi mitandaoni, mpate habari, elimu na burudani katika ubora na kasi ya hali ya juu. Hakika, TTCL imerejea, msisubiri kuhadithiwa, fanyeni maamuzi sasa. Hakikisheni kuwa mnakuwa miongoni mwa wale wanaofaidika na huduma bora za TTCL ambazo zina thamani halisi ya fedha zenu,"

Michuano hiyo iliyoratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kupitia kocha wa taifa wa mpira wa ufukweni nchini ikiwa na lengo kupata wachezaji chipukizi wa mchezo huo ilishirikisha vyuo vya CBE, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo cha IFM, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha NIT, DIT, TIA, Chuo cha Kodi cha TRA -ITA na Chuo cha Ardhi. Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) ndio kiliibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TFF.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)