Pages

MO DEWJI FOUNDATION YATOA MSAADA WA VITANDA, MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuboresha hudumza za afya kwa mama na mtoto, Taasisi ya MO Dewji imetoa msaada wa vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 100 kwa Hospitali ya SekouToure iliyopo mkoani Mwanza. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema msaada huo ni sehemu ya malengo ya taasisi hiyo ya kuhakikisha inasaidia sehemu zenye uhitaji katika sekta ya afya, elimu na ustawi wa jamii. Amesema msaada huo unalenga kusaidia kupunguza vifo vya wanawake na watoto kwani kwa sasa idadi ni kubwa hivyo msaada huo utawezesha mkoa wa Mwanza kuongeza kasi ya mapambano ili kumaliza kabisa vifo vya wanawake na watoto. 
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza kuhusu juhudi ambazo zinafanywa na taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia jamii na malengo ya kutoa msaada katika Hospitali ya Sekou Toure.

"Tunafahamu kwamba asilimia 32 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinatokea katika siku 28 za mwanzo lakini pia tunaelezwa kuwa kila mwaka cha wanawake 8,000 hufariki dunia wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika na sisi kitu cha kwanza tunachotaka ni kusaidia mapambano ya kupunguza vifo vya watoto na wanawake," amesema Barbara. Nae mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameitaja Taasisi ya MO Dewji kuwa mfano wa kuigwa kwa msaada ambao wameutoa kwa hospitali ya mkoa huo na kuwaomba kuendelea kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada zaidi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumzia mipango ya Serikali kuboresha huduma za afya lakini pia kuishukuru Taasisi ya MO Dewji kwa msaada ambao wamewapatia.

"Ukimpa mama afya bora, umesaidia jamii nzima, jambo lililofanywa na Taasisi ya MO Dewji ni kubwa sana, hospitali zetu zinamahitaji makubwa sana na kwa hili ambalo wamefanya ni mfano wa kuigwa na watu wengine, tunawashukuru sana na tunawaomba muwe tayari kutusaidia kwa muda mwingine," amesema Mongella. Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota amesema aliomba Taasisi ya MO Dewji kuwasaidia baada ya kuona changaoto nyingi ambazo zinawakabili wanawake ambao wanakwenda kujifungua katika Hospitali ya Sekou Toure na watoto ambao wanazaliwa.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota akieleza sababu ya kuiomba msaada Taasisi ya MO Dewji ili iwasaidie vitanda, magodoro na mashuka kwa ajili ya wodi ya wazazi.

"Rais Magufuli alikuja hapa na hata yeye aliona changamoto ambazo zinatukabili na mimi kama mbunge niliamua kwenda kuzungumza na watu wa MO Dewji Foundation na napenda kuwashukuru kwa kukubali kutusaidia na naamini msaada huu utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinatukabili," alisema Lwota.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi akitoa taarifa ya Hospitali ya Sekou Toure.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi amesema hospitali hiyo licha ya changamoto ambazo zinawakabili inahudumia wagonjwa 500 kwa siku na kwa wanawake ambao wanafika kujifungua kwa siku wanakadiriwa kuwa kati ya 30 na 40.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipokea msaada wa vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 100 kutoka Taasisi ya MO Dewji.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akimshukuru Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez kwa msaada ambao wamewapatia.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dk. Rweyendela Onesmo akitoa neno la shukrani.Mmoja wa wanawake ambao wamejifungua katika Hospitali ya Sekou Toure, Eveline Francis akiishukuru MO Dewji Foundation kwa msaada ambao wametoa kwenye hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota na Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez wakimjulia hali Zuwena Mohammed baada ya hafla ya kukabidhi msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa UWT Mwanza, Ellen Bagohe na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi wakiwa katika picha ya pamoja.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa UWT Mwanza, Ellen Bagohe na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hospitali ya Sekou Toure.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota.
Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)