Pages

WATANZANIA WAUNGANA NA VIJANA KUTOKA ZAIDI YA NCHI 19 AFRIKA, KATIKA MKUTANO WA MASWALA YA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NAIROBI, KENYA

Kati kati ni Bi. Victoria Mwanziva akiwa na watanzania wengine walioshiriki katika mkutano huo Bw.Innocent Makota na Raymond Paul
Bi.Victoria Mwanziva akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Boniface Mwangi ambaye ni Mwanaharakati nguli wa Kenya anayepinga Rushwa na aliyekuwa mmoja wa wazeshaji katika semina hiyo akimkabidhi nakala ya Kitabu chake Victoria kinachoitwa Unbounded.
Mwanaharakati na mwanamaendeleo nguli kutoka Gambia Bw. Ibrahim akiwa na Bi. Victoria Mwanziva  katika Mkutano huo


Na Mwandishi wetu
Novemba 22-26 mwaka huu 2016 mtanzania Mwanaharakati Bi. Victoria Mwanziva pamoja na watanzania wengine walipata nafasi ya kuhudhuria mkutano maalum wa vijana na maswala ya Demokrasia, maendeleo na ushirikishwaji ulioandaliwa na International Regional Office nchini Kenya jijini Nairobi wakishirikiana na Open Society Initiative East Africa. Hii ilikuwa ni siku chache baada yeye kutoka Addis Ababa Ethiopia ambapo alikuwa mtanzania pekee aliyewakilisha katika mafunzo maalum ya wanawake kwa ajili ya kudumisha Amani Barani Afrika.

Katika mkutano huo kulikuwa na vijana takribani 30 kutoka katika Nchi zilizokadiliwa kuwa 20 Afrika nzima waliotoka katika nyanja tofauti ambao walikuwa na malengo ya chanya ya kuona mbali na maono mema katika nchi wanazotokea.

Katika Mkutano huo Tanzania ilikuwa ni Mfano Bora na iliwakilishwa vema na vijana wake, wakichambua changamoto zao na kupendekeza njia bora za kuzitatua na kuepukana kulaumu na kuendelea kujaribu kukwepa majukumu yanayosababisha nchi zisipige hatua.

"Nachojivunia ni Amani ya Tanzania na jinsi ambavyo nchi yetu inasonga mbele katika kujiinua zaidi na zaidi, Amani yetu inatupa uwanja wa kujiendeleza . Kuna baadhi ya nchi shiriki vijana wao wanalalamika kuwa hata uwepo wa asasi za vijana ni changamoto, lakini nchini Tanzania Asasi zipo na zinainua vijana natamani vijana tuelekeze nguvu zetu katika kuinua na kupeana fursa za kusonga mbele kama Taifa kiujumla" alisema Victoria.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)