Pages

TSN YAADHIMISHA MIAKA 10 YA GAZETI LAKE LA HABARILEO

 Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Wachapaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo imeadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwa gazeti la Habarileo mnamo Desemba 21,2007 kwa kukata keki huku Uongozi wa Kampuni hiyo ukitangaza shamra shamra za mwezi mmoja wa kusherehekea kuzaliwa kwa gazeti hilo.

Aidha ili kushirikiana na wadau wengine, Kampuni imetangaza punguzo la asilimia 30 kwa mteja atakeatangaza tangazo lake ndani ya siku 30 za shamrashamra katika gazeti la Habarileo.
 Miongoni mwa wageni maalum waliohudhuria sherehe hizo ni Mhariri Mtendaji wa zamani wa TSN, Isack Mruma (wapili kulia) ambaye kwa sasa ni Ofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambaye alishiriki kukata keki pamoja na Mhariri Mtendaji wa sasa Dk Jim Yonaz (wapili kushoto) na Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah. Kushoto akishuhudia ni Meneja Mauzo na Masoko, Januarius Maganga. 
 Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah akimlisha keki Kaimu Mhariri wa Gazeti la Habarileo, Nicodemus Ikonko.
 Shangwe za miaka 10 ya Habarileo.
 ME wa zamani wa TSN Isack Mruma akilishwa keki na ME wa TSN Dk Jim Yonazi.
 Ilikuwa ni furaha sana kwa viongozi hawa .
 Isack Mruma akimlisha keki Dk Jim Yonazi.
 Isack Mruma akizungumza katika shamra shamra hizo na kuelezea changamoto mbalimbali alizokumbana nazo tangu kuanza kwa gazeti hilo.
 Wafanyakazi wa TSN wakifuatailia
 Mruma akizungumza na viongozi wa TSN kumsikiliza kwa makini.
 Isack Mruma akiagana na wafanyakazi wa gazeti la Habarileo ambao wengi wao alianza nao gazeti hilo.
 Dk Jim Yonazi (kushoto) akimsindikiza Isack Mruma
Picha ya pamnoja ilipigwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)