Afisa wa jeshi la polisi kitengo cha Usalama ,Haji Nduya akitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kanda maalum ya Dar es Salaam chini ya udhamini wa TBL Group, ikiwa mkakati wa n kupunguza ajali za barabarani.
Afisa masuala endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Oysterbay jijini ya Dar es salaam wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi (kulia) na Afisa wa Masuala Endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kushoto)wakitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi akiowaongoza wanafunzi wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, kuvuka barabara ya Haile Selassie, kwa kutumia alama za barabarani (zebra).
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi akiowaongoza wanafunzi wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, kuvuka barabara ya Haile Selassie, kwa kutumia alama za barabarani (zebra).
Afisa Mawasiliano wa TBL Group, Amanda Walter akimkabidhi zawadi ya mkebe wenye vifaa vya shule mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jesca Reginald mara baada ya kujibu maswali yaliyohusu usalama wa barabarani, wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama Kanda maalum ya Dar es Salaam,yaliyodhaminiwa na TBL Group ikiwa ni sehemu ya kupunguza ajali kwa watoto wa shule wakati wanapovuka barabara wakienda au kutoka shuleni.Kushoto ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi.
-Yamedhaminiwa na TBL
Katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki Jeshi la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni liliendesha mafunzo ya usalama barabarani katika shule ya msingi Oysterbay chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
Wakati wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na askari kutoka Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani wanafunzi waliweza kufundishwa alama mbalimbali za bararani,mambo ya kuzingatia wanapokuwa barabarani na jinsi ya kuvuka barabara kwa tahadhari.
Pia wanafunzi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na waliulizwa maswali ya chemsha bongo kuhusiana na elimu ya mafunzo waliyopatiwa.
Afisa mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter, alisema kuwa TBL imedhamini mafunzo haya ikiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za serikali za kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kampeni za usalama barabarani.
“Kampuni ya TBL tunao mkakati wa kuendelea kushirikiana na serikali kupitia kikosi cha Polisi wa Usalama barabarani na wadau wengine kuhakikisha tunapunguza matukio ya ajali za barabarani nchini ambazo zimekuwa zikisababisha vifo,ulemavu na hasara kwenye jamii”.Alisema.
Alisema mpango wa kuwafikishia wanafunzi wa shule za msingi elimu ya usalama barabarani hauna budi kuungwa mkono kwa nguvu zote kwa kuwa wakielewa tatizo hili mapema itakuwa ni rahisi kutokomeza tatizo hili katika siku za usoni. “Wanafunzi wana uelewa mkubwa na ni rahisi kushika wanayofundishwa pia wanaishi katika mazingira ambayo ni muhimu kuwa na ufahamu wa masuala haya”.
Mbali na kudhamini mafunzo haya ya wanafunzi kampuni ya TBL Group imekuwa mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Nenda Kwa Usalama ngazi ya kitaifa ambapo ilitoa vifaa mbalimbali vya uhamasishaji ikiwemo gari maalumu ya kupimwa afya za madereva la Zahanati inayotembea maarufu kama ‘Zahanati Mwendo’,huduma ambayo ni ya kwanza nay a aina yake nchini ambayo mpaka sasa inaendelea kuchangamkiwa na madereva popote linapopita gari hilo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)