Pages

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATEMBELEA BANDARI YA TANGA

Tanga, WAJUMBE 14 wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi Baraza la Uwakilishi  la Zanzibar wamesema  ujio wa  Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga  litaongeza ajira kwa vijana wakiwemo Wanzanzibar waishio Tanga.
Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea  bandari ya Tanga eneo la upakuzi wa shehena ya mizigo na eneo itakapojengwa bandari mpya ya Mwambani.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo,  Hassan alisema Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari zake ikiwemo ya Wete na Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Bomba la Mafuta.
Akizungumzia  kilio cha wafanyabiashara na wasafiri wa Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri wa baharini, Hassan alisema kero hiyo Serikali inaitambua na jitihada za kuwa na meli ya uhakika inafanywa.
Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa wakichukua bidhaa Tanga wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika wa baharini.
Awali akizungumza na wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi, Kaimu Meneja wa Badari Tanga, Henry Arika, alisema mchakato wa mradi wa bomba la mafuta unaenda kwa kasi na kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja kuwekeza.
Alisema Tanga ziko fursa nyingi za uwekezaji  na yako maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa mradi wa Bomba la mafuta amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia.
                                   
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe 14 wa Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar walipotembelea bandari ya Tanga kujifunza 


  Afisa Mtekelezaji Mkuu Bandari ya Tanga, Donald Kaire, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar walipofanya ziara bandari hiyo juzi. Katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)