Pages

TANAPA NA WADAU WA USAFIRI WA ANGA KUKUZA SEKTA YA UTALII NCHINI

Ndege ya shirika la Precision Air ikiwa tayari imetua katika uwanja wa Seronera ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoa wa Mara ikiwa na watalii 43 kutoka nchi Afrika Kusini iliyowachukua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hatua inayoelezwa kuokoa muda na kupunguza gharama.

Abiria wakishuka kutoka kwenye ndege ya shirika la Precision Air ambayo imeanza safari za moja kwa moja kutoka jijini Dar es Salaam na Zanzibar hadi kwenye hifadhi hiyo.

Watalii wakifurahi baada ya kutua salama kwenye uwanja wa Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(katikati)akiwa katika picha ya pamoja wa wafanyakazi wa shirika la Precision Air,kulia kwake ni Kapteni Benjamini Maluli na kushoto kwake ni Murtazir Ghulamhusein


Watalii wakipata picha ya pamoja ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete akifafanua umuhimu wa ndege kubwa za abiria kwenda moja kwa moja kwenye hifadhi za taifa kutakavyoinua sekta ya utalii nchini.

Ndege ya shirika la Precision Air ikiruka kutoka uwanja mdogo wa Seronera  ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoa wa Mara.

Makundi makubwa ya wanyama aina ya Nyumbu ni miongoni mwa vivutio ndani hifadhi ya Serengeti

Tembo wenye miili mikubwa wakiwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti

Fisi wakijipooza joto kwenye dimbwi la maji.



Wafanyakazi wa Sence of Afrika wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa tayari kuwapokea wageni wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)