Pages

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI FINLAND

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe. Vesa Viitaniem (kushoto) masuala mbali mbali ya uwekezaji,elimu na uwezeshaji Ikulu jijini Dar es Salaam, katikati ni  Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote Mama Anna Mkapa .


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Mhe.   Vesa Viitaniem (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.


                          ............................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya Finland kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem



Makamu wa Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa Serikali ni kuhakikisha taifa linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali Duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na kuwezesha makundi mbalimbali ya kijamii hapa nchini ikiwemo ya wanawake,yatima na vijana.

Makamu wa Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote nchini.

Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya

kazi zao kwa ufanisi.


Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.

Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland Vesa Viitaniem aliongozana na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)