Kama wewe ni mhitimu katika Uhandisi au Utawala (Masoko,
Mahusiano, Fedha) na una ari ya kujifunza, ukiwa na mtazamo chanya wa mafanikio
na mfuatiliaji wa maadili katika kazi, njoo ujiunge nasi katika bonanza hili la
uchambuzi wa ajira.
Rasilimali Watu
Mauzo
Uhasibu
Masoko
Uhandisi
Kilimo
Nguo
Kwani unaweza ukawa mmoja kati ya watu 25 tutakao wachagua
kwa ajili ya kujiunga kwenye programu ya uendelezaji wa wahitimu wa vyuo vikuu.
Na ukibahatika kuwa mmoja wapo kati ya hao utapata nafasi ya
kujifunza kwa vitendo katika viwanda vyetu vilivyopo maeneo mbalimbali.
Pia utapata nafasi ya kufundishwa mifumo ya uendeshaji wa
viwanda vya kisasa.
Utakuwa chini ya wakufunzi waliobobea katika kazi zao
duniani ambao watakuwezesha wewe kukua
katika kazi na kushika nyadhifa kwenye kazi yako.
Zaidi ya yote hayo utakayofanyiwa pia utalipwa ili kujifunza
Kwa taarifa zaidi tazama vipeperushi vyetu:
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)