Pages

MBUNGE COSATO CHUMI AANZA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI

Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akikagua pump kwenye moja ya kisima kwenye shule ya Msingi Makalala, anayetizama ni Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi

 Bw Donsun Lee ambaye ni Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International akimsikiliza kwa makini Mhandisi wa Maji wa Mji wa Mafinga Eng Eradius.

 Pichani baadhi ya wanafunzi na waalimu wa shule ya Msingi Makalala wakiwa katika picha ya pamoja na Mrs Lee  na Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi

 na fredy mgunda,iringa


MBUNGE wa jimbo Mafinga mjini Cosato Chumi ameendeleza juhudi zake za kuwatafutia maendeleo wananchi wa jimbo lake kwa kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali za nje ya nchi ya Tanzania pamoja na taasisi za ndani.


Hivi karibu balozi wa korea nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya Kutoka Korea ya World share  alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea changamoto za jimbo hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya  changamoto hizo na walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.


Baada ya balozi huyo kurudi jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo ambazo alikuwa amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.


Aidha mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua kwa kuwa ameshazifanyia utafiti.


“Leo nimetembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga na nimejionea shida ya upatikanaji wa maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun Lee.


Bw Donsun Lee alimpongeza mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za kuwashawishi kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto  ambazo wanaweza kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.


Katika ziara hiyo Bw Lee na timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga. Aidha baada ya tafiti hizo, Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya Serving Friends International huko Seoul, Korea.


Nia ya kufanya tafiti hizo ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa sababu ndo utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani Singida


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa kufanikisha kufanya tafiti ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na taasisi hiyo.


Chumi ameongeza kuwa haya ni matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea jimbo la Mafinga Mwezi mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.


Lakini mbunge Chumi amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma na kuunganisha na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi inayotakiwa.


“Unakuta mbunge nahangaika kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini ukienda vijiweni unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga soga zisizo na malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la mafinga mjini litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)