Pages

DC STAKI: APIGA MARUFUKU KUFANYA BIASHARA KWA KUJAZA RUMBESA

Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akikagua magunia yaliyokutwa yakiwa yamejazwa Rumbesa
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akizungumzia unyonyaji wanaokumbana nao wananchi kutoka kwa wafanyabiashara wanaotaka magunia yaliyojazwa Rumbesa
Gari aina ya Fuso likiwa limekamatwa mara baada ya kubainika kuwa limebeba magunia ya vitunguu ambayo yamejazwa Rumbesa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wananchi Wilayani humo
 Dc Staki akikagua mashamba ya wakulima mara baada ya kuzuru katika maeneo hayo
 Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo wakisikiliza malalamiko ya wananchi

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Wakulima wa mazao mbalimbali likiwemo zao la vitunguu wametakiwa
kutofanya biashara kwa kujaza rumbesa ili kuwanufaisha wafanya biashara
ambao wanajitokeza vijijini kunua mazao kwani jambo hilo linawanyonya
zaidi wakulima na kuwanufaisha wafanya biashara.

Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
Rosemary Staki Senyamule mara baada ya kuitisha mkutano wa wananchi
katika ziara yake ya kuwahimiza kwa pamoja kujitokeza kushiriki katika
zoezi la upimaji ardhi linaloendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Same.

Hata hivyo lengo mahususi la kuamua kuwapo kwa zoezi la upimaji ardhi
ni kutaka kuondoa migogoro ya ardhi iliyokithiri katika maeneo
mbalimbali Wilayani humo sambamba na kupinga kipimo cha Rumbesa
kinachowanyonya wakulima wengi nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika Katika Kitongoji cha Jitengeni na Mvungwe
uliwahusisha pia wataalamu wa kilimo na ardhi kutoka katika Halmashauri ya Wilaya hiyo sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo.

Katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wakazi wa Kijiji cha Ruvu Jiungeni kushiriki kikamilifu katika zoezi la upimaji ardhi hivyo kuwaarifu pia wananchi wote kujitokeza katika mashamba yao wakati wa zoezi la upimaji ili kuondoa adha inayochochea
migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Dc Staki alisema kuwa wananchi wanapaswa kupinga kuzidisha kipimo halisi kinachokubalika kwani kutofanya hivyo ni kukubali kupunjwa na kuinyima Halmashauri mapato.

Alisema kuwa wakulima wanapaswa kujiamini kwani mazao wanayolima yana soko popote nchini hivyo kidanganywa kwa kuweka Lumbesa ni kujinyima haki yao ya msingi katika kukabiliana na wimbi la umasikini.

Aidha kabla ya mkutano na wananchi Dc Staki alitembelea mashamba ya vitunguu na kujionea jinsi ambavyo Rumbesa inavyofungwa.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya alimtaka mkuu wa Polisi Wilaya ya Same Asteriko Maiga kusimamia na kulikemea suala la Rumbesa kwenye mageti yote na endapo watawabaini wafanya biashara wanaofanya hivyo wanapaswa kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anna-Claire Shija alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini katika kuimarisha kilimo na kujitokeza kwa wingi katika shughuli za maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)