Meneja Ugawaji wa huduma za TBL Group,James Nyoike,amesema kuwa utumiaji wa vifaa bora na vya kisasa unapunguza matukio ya ajali sehemu za kazi hususani viwandani na kuongeza ufanisi wa kazi na kuongeza uzalishaji.
Bw.Nyoike aliyasema hayo wakati wa kupokea magari ya kupakia na kupakua mizigo (Forklifts) za kisasa zilizonunuliwa na kampuni hiyo kutoka kampuni ya kusambaza vifaa vya viwandani ya Effco Solution Limited.
Alisema kampuni ya TBL Group inao makakati kuhakikisha inatumia mitambo ya kisasa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kulinda usalama wa wafanyakazi wake ikiwemo kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji “Tunapoongelea vifaa vya kisasa hatumaanishi mitambo tu bali hata vifaa vyote vinavyotumika katika kazi ikiwemo magari yanaotumika kusambaza bidhaa zetu na yanaotumiwa na wafanyakazi wetu katika shughuli mbalimbali “.Alisema.
Dereva akiendesha moja ya Forklift nne za kisasa zilizonuliwa na kampuni
Madereva wa Forklift wakiwa wanajaribu kuziendesha baada ya kukabidhiwa
Meneja Ugavi na Usambazaji wa TBL Group ,James Nyoike ( wa Nne kutoka kulia) na madereva wa kuendesha Forklifts wakimsikiliza mtaalamu kutoka EFFCO Solution Donald Luvaga (kushoto), jinsi Forklift za kisasa aina ya Toyota zilizonunuliwa na kampuni ya TBL zinavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)