Pages

Timu ya JamiiForums yapata ajali maeneo ya Mbaoni - Urambo

Tunasikitika kutangaza kutokea kwa ajali ya timu (2) ya wana Jamii Media, waliopo kwenye safari za mradi wa TUSHIRIKISHANE (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") iliyotokea hapo jana saa 5 asubuhi, maeneo ya Mbaoni - Urambo (Tabora). Timu hiyo ilikuwa na Meneja Uendeshaji na Mikakati wa Jamii Media, Bi Asha D. Abinallah na Mshauri wa Miradi Bw. Ericus Kimasha.

Timu hiyo ilikuwa ikielekea Kigoma mjini ili kukutana na wenzao ambako walikuwa na ratiba Warsha, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Mradi wa TUSHIRIKISHANE mara baada ya kumaliza shughuli zake hizo jimboni Nzega.

Kwa sasa hali zao si mbaya sana na wapo njiani kurudi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

JamiiForums tunatoa shukrani za dhati kwa wana Urambo kwa Ushirikiano, Matibabu, Ulinzi na Usalama uliyotolewa wakati na baada ya ajali hiyo.

tmp_22015-IMG-20160817-WA0024-2113068098.jpg

tmp_22015-IMG-20160817-WA0020-1711562377.jpg

tmp_22015-IMG-20160817-WA0007983277075.jpg

34bd39ab-0f07-4842-a54a-37ea9ceaf24f.jpgJamii Media inawashukuru Sana Bw. na Bi. Banyanga, wamiliki wa Magole Pre & Primary School kwa kuwasaidia wafanyakazi wetu waliopata ajali
82b69bf8-ce78-4faa-a8a7-ed6178700527.jpg
Jamii Media inawashukuru Afande Jonas na Afande Abdallah wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilayani Urambo kwa msaaada na huduma ya haraka kwa wafanyakazi wetu.JamiiForums​

OUR NOTE:
Lukaza blog inapenda kutoa pole kwa timu nzima ya Jamii Media kwa ajali iliyowakumba wafanyakazi wake lakini Pia inapenda kumshukuru Mungu kwa kuwanusua kwenye ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)