Pages

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa  maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho  kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)  Pascal Shelutete  akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa  habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum  kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi . 

Na Dixon Busagaga ,Mbarali,Mbeya . 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio  la kupatwa  kwa jua  linalotarajia kuonekana Septemba mosi  mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha 

Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete  anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni  fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa  eneo la Ihefu  linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo   ina vivutio vingi, hivyo amewataka  wananchi watakaofika kuangalia
kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga
Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)