Pages

Rio2016: Mkenya Eliud Kipchoge ashinda mbio za marathon

Eliud Kipchoge wa Kenya ahsinda mbio za marathon

Image captionEliud Kipchoge wa Kenya ahsinda mbio za marathon
Mkenya Eliud Kipchoge aliwaacha wenzake wakimfuata nyuma kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.
Kipchoge mwenye umri wa miaka 31 ambaye alishinda mbio za London Marathon mnamo mwezi Aprili alitawala mbio hizo na kumaliza katika muda wa saa mbili,dakika nane na sekunde 44.
Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 ili kushinda fedha naye raia wa Marekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.
Ushindi huo sasa unaipatia kenya medali yake ya sita kabla ya kukamilika kwa michezo hiyo siku ya Jumapili.
Kenya pia ilijishindia medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanawake katika siku ya kwanza ya mashindano hayo ambapo Jemimah Sumgong aliibuka mshindi.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)