Pages

ORODHA YA MAJINA YA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU WANAOTAKIWA KUONANA NA MADAKTARI BINGWA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UPIMAJI AFYA KWA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU
Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) utaendesha zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu ambao waliachishwa kazi na mgodi huo mnamo mwaka 2007 bila kupimwa afya zao kinyume na Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.


Baada ya ukikwaji huo wa sheria kuripotiwa kwa Wakala, hatua stahiki zilichukuliwa ikiwemo kufanya kaguzi maalum za usalama na afya katika eneo la mgodi na kutoa onyo kali kwa mwajiri wa walalamikaji pamoja na kugharimia upimaji afya za waathirika wote.

Katika kushughulikia tatizo hilo, vikao vya mashauriano vilivyojumuisha serikali, mwajiri (Mgodi wa Bulyanhulu) na waathirika kupitia chama chao, TAMICO, vilifanyika na utaratibu wa kushughulikia suala hilo ukawekwa. 

Katika utaratibu huo, TAMICO ilipewa jukumu la kuwatafuta waathirika wote popote walipo na kuwasilisha majina yao kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi. 

Wakala ulikuwa na jukumu la kuyapeleka majina hayo kwa mwajiri kwaajili ya uhakiki na kuratibu upimaji afya wa waathirika hao baada ya majina yao kuhakikiwa. 

Hadi kufikia sasa tayari waathirika 315 kati ya 371 ambao mwajiri alithibitisha kwamba walikuwa wafanyakazi wake wameshapimwa afya zao. 

Waathirika 56 waliobaki hawakujitokeza wakati wa upimaji afya licha ya kupewa taarifa juu ya zoezi hilo.  

Waathirika watakaopimwa kwasasa ni wale ambao vipimo vyao vya awali vilionesha kwamba wanahitaji vipimo zaidi kutoka kwa madaktari bingwa. 

Maandalizi ya upimaji huu yamekamilika na zoezi hili litafanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku ya Jumamosi tarehe 20/08/2016 na katika hospitali ya rufaa ya Bugando mnamo tarehe 22/08-15/09/2016.

 Katika zoezi hili waathirika ambao orodha ya majina yao imeambatanishwa katika taarifa hii wataonana na madaktari bingwa wa magonjwa ambayo wana dalili nayo ili kubaini kama wana matatizo kiafya na hatimaye kuweza kutazama kama matatizo waliyo nayo yametokana na kazi walizokuwa wakifanya mgodini. 

Kwa waathirika ambao madaktari watathibitisha kwamba matatizo yao ya kiafya yamesababishwa na kazi walizokuwa wanafanya, Wakala utashauri namna ambavyo wanapaswa kufidiwa kwa mujibu wa sheria za nchi. 

Waathirika ambao watakutwa na matatizo ya kiafya ambayo hayatokani na kazi, watashauriwa kuendelea na matibabu katika hospitali zilizopo karibu nao.

Aidha kwa waathirika ambao hawatakutwa na matatizo yoyote ya kiafya watapatiwa vyeti vyao (certificate of fitness) ambavyo hutolewa kwa wafanyakazi wanaopimwa afya zao baada ya kukoma kwa ajira zao kwa mujibu wa kifungu Na.24 (2) cha Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

Ikumbukwe kwamba, upimaji huu ni mwendelezo wa hatua mbali mbali zinazochukuliwa na serikali katika kushughulikia tatizo hili ambalo lilitokea mwaka 2007 ambapo waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu waliachishwa kazi na mwajiri wao baada ya kugoma kufanya kazi. 

 Hata hivyo mwajiri wao (Mgodi wa Bulyanhulu) haukuweza kuwapima afya zao kama Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 inavyomtaka.

Mwisho, kwakuwa suala hili ni la kisheria na serikali ina nia ya dhati ya kulishughulikia, tunaomba ushirikiano kutoka pande zote (waathirika na mwajiri) ili kuhakikisha kwamba zoezi hili linatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Imetolewa na;

Dkt. Akwilina Kayumba
Mtendaji Mkuu


ORODHA YA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU AMBAO WATAONANA NA MADAKTARI BINGWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI NA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO (MWANZA)

A: MUHIMBILI-DAR ES SALAAM; 20/08/2016 (MUDA SAA 3: 00 ASUBUHI)
NA.
JINA LA MFANYAKAZI
1
JUMA SAID MANGU
2
ENOS TABAN BUPAMBA
3
SALUM KANANI SIMBEYE
4
ANITA JONAS NGONYANI
5
MBAZI SHUDI MRUTU
6
VICENT MICHAEL MASUKE
7
MABULA E. MANYANYA
8
SIMON AJABUELI NGOYE
9
GENDO RAMADHANI KIBWENGO
10

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)