Pages

NEWS ALERTS: ASKARI POLISI WATATU WAUWAWA USIKU HUU HUKO MBAGALA

Taarifa iliyotufikia usiku huu inaeleza kuwa, kuna tukio la kuuwawa kwa Askari Polisi, lililotokea huko Mbagala jijini Dar.

Inadaiwa kuwa askari hao wali kuwa wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi na kuanza kuwashambulia kwa risasi na baada ya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki wakielekea maeneonya Mvuti.

ASKARI WALIOFARIKI ni
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO.

Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 ni katika tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE na inadaiwa kuwa wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.

Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva.

Inadaiwa kuwa watu hao hayakuingia ndani ya bank.

Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa sana kwa risasi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)