Pages

Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla afanya ziara Hospitali ya Wilaya ya Bukombe

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe I liyopo Mkoani Geita sambamba na kukutana na watumishi wa sekta ya Afya ambapo ametoa maagizo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za Afya hapa Nchini.

Akiwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo ya Bukombe, aliweza kubaini mapungufu mbalimbali ikiwemo jengo la chumba cha Upasuaji ambapo amewaagiza wafanyie marekebisho ya haraka ili kuiweka katika kiwango cha ubora unaotakiwa.

Aidha, ameuagiza uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanafunga mifumo ya malipo ya kielektroniki na ndani ya miezi sita wawe wanatumia mfumo huo na si kupokea pesa mkononi.

“Naagiza. Kuanzia leo ndani ya miezi mitatu muhakikishe mumefunga mfumo wa malipo kwa njia ya kielekroniki ambapo mfumo huu ufungwe kwenye sehemu zote za ukusanyaji wa mapato. Mapokezi, Mahabara, Chumba cha X ray, Chumba cha upasuaji. Hakika ndani ya miezi mitatu mingine muwe tayari mumeachana na mfumo huu wa kupoea pesa mkononi hivyo baada ya miezi sita mfumo huo ukamilike na hili ni agizo” alieleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha wa kutembelea kituo cha Afya cha Ushirombo ambapo ameagiza wahakikishe wanajenga chumba cha Upasuaji katika moja ya majengo yao ya kituo hicho pamoja na kukarabati vizuri chumba cha Mahabara ili kutoa huduma bora na zenye uhakika kwa wagonjwa ambao wamekuwa ni kimbilio kwenye kituo hicho.

Awali akizungumza na Watumishi wa Idara ya Afya wa Wilaya hiyo, aliwapongeza kwa kazi za kila siku za kuwatumikia wananchi wa Tanzania ambapo aliwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo bega kwa began a inatambua changamoto zao na wanazishughulikia hasa kwa kipindi hiki cha Hapa Kazi.

“Serikali inatambua changamoto kwa watumishi wa Afya. Ndio maana hata bajeti ya mwaka huu ndani ya Wizara yetu imeongezeka mara dufu. Tuwatumikie wananchi, tufanye kazi kwa moyo na kero na matatizo yote tunayashughulikia. Sikutaka kukaa Ofisini na kutuma watendaji wa Wizara bali nakuja mimi mwenyewe kujionea changamoto hizi” alisema Dk. Kigwangalla.

Hata hivyo ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Bukombe na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanashughulikia malipo ya watumishi hao wa Afya pamoja na watumishi wengine haraka iwezekanovyo kwani imebainika kuwa, Wao na Madiwani hawana matatizo huku wakilipana stahiki zao kwa wakati ila watendaji wengine wao wanapata taabu.
DSC_7158Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amabye alifika kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Bukombe Agosti 20.2016
DSC_7160Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Watumishi wa Idara ya Afya wa Bukombe (hawapo pichani)DSC_7154
Baadhi ya watumishi wa Idara ya Afya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa mkutano huo
DSC_7156
Baadhi ya watumishi mbalimbali wakiwemo wa Afya na Wilaya ya Bukombe wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
DSC_7181
Ugeni ukiwasili kwenye kituo cha Afya cha Ushirombo kilichopo Wilayani Bukombe Mkoani Geita.
DSC_7177
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo ya namna watakavyoboresha kituo hicho cha Afya kwa upande wa Chumba cha upasuaji na sehemu ya MahabaraDSC_7171Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Dk. Kazuzu wa Kituo cha Afya Ushirombo (kulia) namna atakavyoboresha chumba cha Mahabara na Upasuaji. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo ya Bukombe. DC Maganga.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)