Pages

MKUTANO WA LOWASSA NA WANAFUNZI MUHIMBILI WAZUILIWA

Na Dotto Mwaibale

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mkutano uliokuwa ufanywe na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowaasa.

Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike na baadhi ya vijana wa kikristo ambao ni wanafunzi wa chuo hicho ulikuwa pangwa kufanyika juzi chuoni hapo kuanzia saa za mchana.

Akizungumza mtandao wa www. habari za jamii.com  mmoja wa wanafunzi hao ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema maandalizi yote ya mkutano huo ambao ulikuwa baada ya ibada yalikuwa yamekamilika.

"Tulifanya taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo ambao ulitukubalia na kumualika ndugu Lowassa lakini tumeshangazwa na zuio lililotolewa na uongozi wa chuo" alisema mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo alisema kuwa saa sita mchana wakati wakimsubiri mgeni rasmi Edward Lowassa awasili mkuu wa chuo hicho na viongozi wengine waliwaita na kuwaeleza kwamba mkutano huo umewekewa zuio kutoka juu hivyo hautafanyika bila ya kutoa sababu .

Msemaji wa Lowassa Abubakar Lihongo alisema wanafunzi hao baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano huo walimuomba radhi Lowassa na kumueleza watamualika tena kipindi kingine wakiwa tayari.

"Mimi naona zuio hilo linatokana na masuala ya kisiasa lakini kuna barua ya wanafunzi hao ipo katika mitandao ya kijamii mkiipata mnaweza kupata picha halisi" alisema Liongo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)