Pages

MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND


Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bwa. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT. 
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa
wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti 2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya
zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini yamiradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa Halmashauri husika.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bwa. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bwa. Peter Ireton .
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar,Dkt Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)