Pages

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA APONGEZA JUHUDIZA WAKULIMA NA WATAFITI WA KILIMO

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha maadhimisho 23 ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Sehemu ya Wakazi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Lindi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Luteni Joseph Benedict Lyakurwa wa Suma JKT   alipotembelea eneo lao na kujionea shughuli mbali mbali za kilimo na ufugaji kwenye kilele cha maadhimisho ya 23 ya sikukuu ya wakulima ya   Nanenane mkoani Lindi


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Daraja la kwanza Halima Kikwega wakati wa  kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane Ngongo Lindi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia wananchi mikono wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho ya Wakulima Nane nane mkoani Lindi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewahakikishia watanzania kuwa serikali ya awamu ya TANO inadhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii kwa kuendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi,kudhibiti matumizi yasiyolazima, kuimarisha mifumo  ya ukusanyaji wa kodi ili fedha zinazokusanywa zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.


Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya


sikukuu ya Wakulima Nane Nane kitaifa katika uwanja wa Ngongo Manispaa ya Lindi mkoani Lindi kwa naiba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 

Katika hutoba yake kwa mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya Ngongo, Makamu wa Rais amesema azma ya serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo itatimia iwapo tu wananchi wataunga mkono jitihada za serikali katika kulipa kodi kwa wakati,kudai risiti,kufanya kazi kwa bidii, kukemea vitendo vya rushwa kama hatua ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020.


“Napenda kuwahakikishia kuwa tuna dhamira ya dhati ya kuendelea kuwatumikia na kuwaboreshea huduma zote za kijamii pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla bila kujali mikoa mnayotoka,jinsia,dini au itikadi za vyama vyenu.”


Kuhusu uimarishaji wa shughuli za kilimo nchini, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu  Hassan amesema maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane ni moja katika ya juhudi  za serikali za kuboresha shughuli za kiuchumi katika taifa ambapo asilimia 75 ya wananchi wanajihusisha na shughuli za kilimo,mifugo na uvuvi kote nchini.


Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuzipa  kipaumbele sekta za kilimo,mifugo na uvuvi na kuongeza bajeti katika sekta hizo ili ziweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi kwa ujumla.


Makamu wa Rais ameeleza wananchi kuwa serikali imeweka mikakati na mipango inayolenga kusaidia uimarishaji wa shughuli za kilimo kote nchini kwa kuongeza matrekta makubwa na madogo kutoka 7,491 mwaka 2005/2006 hadi 16,478 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 hivyo kupunguza matumizi ya jembe la mkono kutoka asilimia 70 hadi asilimia 12.



Aidha amefafanua kuwa serikali imeongeza idadi ya maafisa ugani katika kilimo kutoka 3,379 mwaka 2005 hadi 2006 hadi 8,756 mwaka 2015/2016 na serikali pia imefufua mashamba ya mbegu kwa kuhusisha sekta binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika kuzalisha mbegu bora za mazao ya chakula nchini.


Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amehimiza wananchi kote  nchini kulipa kodi ipasavyo ili fedha zitakazopatikana zipelekwe kwenye miradi   ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami huku Waziri wa  Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Charles Mwijage akiwataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waongeze uzalishaji wa mazao ya biashara ambayo watauza ndani na nje ya nchi katika hatua ya kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)