Pages

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WAKADIRIAJI MAJENZI AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji  Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini  Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
 Rais wa  Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
 Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji  Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini  Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi  Tanga, Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.

Amesema serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)