Pages

KOREA KUSINI YATOA BILIONI NNE KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance  akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa  wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya  Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa  cha taarifa za hifadhi hiyo.
  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Zara(katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy Chamburo.(kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha  kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa  kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa.
Moja ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake  Prof,Dkt Bernhard Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
  Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Na Dixon Busagaga, Kanda ya Kaskazini. 


Hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti kwa kushirikiana na  serikali  ya  Korea  ya Kusini imeanza mchakato wa ujenzi  wa  kituo  cha  kimataifa cha kutunza tarifa za  mienendo  ya  Wanyamapori kitakachojulikana  kama Serengeti Internatinal Media Centre.



Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi  shilingi bilioni nne kitajengwa
katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .



Tayari  serikali  ya  Korea  Kusini   imeshatuma  wajumbe  wake  kuja  nchini  tanzania  kujionea neneo  kitakapojengwa  kituo  hicho  na  kukamilisha ntaratibu  nyingine  muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung  amesema mradi huo ni mwendelezo  wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.



Akizungumza  na  ujumbe  huo  mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti 
Wiliam Mwakilema  amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu
utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.



Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance  amesema ujenzi utaanza mwezi october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika  baada ya miezi 14.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)