Pages

DALADALA LAPINDUKA KITUONI MBAGALA-SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM, WATU KADHAA WAJERUHIWA

HABARI/PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
DALADALA namba T274 DEX,(pichani), lililokuwa likisafiri kutoka Mbagala RangiTatu kuelekea Temeke jijini Dar es Salaam, limeanguka mita chache kutoka kituo cha Daladala Sabasaba-Mbagala leo asubuhi Agosti 11, 2016 na kujeruhi watu kadhaa. Mashuhuda wanasema, Daladala hilo lililokuwa katika mwendo kasi, liliserereka na kuacha njia wakati likikaribia kusimama kituoni.

Dereva wa Daladala hilo aliruka na kukimbia, nakuwaachaabiria wakitaharuki kila mmoja akijaribu kukoa maisha yake.
“Unajua mvua hizi zilizonyesha asubuhi zinafanya barabara iteleze na hawa jamaa mwendo wao unajua tena, sasa alijaribu kufunga breki gari likaanza kuserereka na alipojaribu kurudi barabarani likakataa na kutumbukia mtaroni,” anasimulia mmoja wa mashuhuda aliyekuwa eneo la ajali.
Polisi wa usalama barabarani alifika muda mfupi baada ya ajali hiyona taratibu ya kuliondoa gari hilo zilianza.

Abiria wote walitoka salama, wachache walijeruhiwa na baadhi yao walionekana wakilia kutokana na mshtuko wa ajali hiyo ya asubuhi.
 Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
  Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
 Wapita njia wakimuuliza abiria huyu (aliyekaa), ambaye alikuwa ndani ya daladala hilo
 Polisi wa usalama barabarani, akikagua mazingira ya ajali hiyo huku akizungumza na simu yake ya mkononi
 Mtu huyu ambaye haikujulikana maramoja kama ni muhudumu wa daladala hilo au abiria akitoka ndani ya daladala hilo baada ya "kupiga mwereka'
 Mashuhuda kama kawaida yao

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)