Pages

BLACKFOX MODELS AFRICA WAFANIKISHA ZOEZI YA KUSAJILI VIJANA WA ARUSHA

Jumapili ilikuwa siku ya furaha kwa wanamitindo wa Arusha, kwani timu ya Blackfox Models ilitua jijini humo kusajili vijana wenye fani hiyo.

Zoezi hili lilifanyika katika hoteli ya Tulia Boutique Hotel and SPA iliyopo Sakina. Miss Aj Mynah, alisema " nimefurahi sana kwa sisi kufanikisha jambo hili, kwani, lengo letu kubwa ni kuendeleza vipaji vya vijana hawa hasa kwenye uanamitindo na hata kwenye mambo ya Arts Vililevile.

Tumeona Arusha ina vipaji vingi sana, na tumekuta kijana mmoja utakuta ana kipaji cha kuimba, uanamitindo, acrobatics na hata kucheza. Kwakweli tumefurahishwa na tutafanya vilivyo kuhakikisha tunakuza vipaji hivi - alisema AJ. Blackfox wamesajili vijana 12 kutoka Arusha, na wameahidi kutembea kwenye miji mingine kusajili.

Blackfox Models Africa, ni Agency ambayo inajihusisha kwenye kusajili vijana na kuwapa mazoezi kwenye uanamitindo, pia kuwatafutia kazi za kwenye uanamitindo nchini. Ofisi yao iko Karibu na ubalozi wa Marekani. Kwa wale vijana ambao wanataka kuingia Blackfox wanaweza kwenda kwenye tovuti yao www.blackfoxmodelsafrica.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)