Pages

Wizara ya Sanaa na Utamaduni hii inawahusu sana katika kuendeleza sanaa nchini

Hivi karibuni tumeshuhudia wasanii wetu hasa wa muziki wa kizazi kipya wakienda nchini Afrika Kusini kwaajili ya Kutengeneza video zao za muziki. Hali hiyo ya kwenda kutengeneza video hizo nchini Afrika Kusini imeonekana sasa ndio kawaida na kila msanii mwenye uwezo wa kutengeneza ataenda Afrika Kusini kwaajili ya Kutengeneza video, Moja ya sababu kubwa inayotajwa kwanini wanaenda Afrika Kusini ni kwamba wanafata watu wenye kutengeneza ubora wa video hizo. Lakini ikumbukwe kuwa hata hapa kwetu wapo watu wenye uwezo wa kutengeneza video bora lakini tukumbuke kuwa video bora inachangiwa na vitu vingi sana kama Madhari (location), Nguo, Wachezaji, Muongozaji, Watu wa Kamera pamoja na vifaa vinavyotumika katika kutengeneza video husika. Kwenda Afrika Kusini kutengeneza video imekuwa gumzo kutokana na wadau wengi kusema kuwa Kunaikosesha Serikali ya Tanzania Mapato kwasababu vitu vyote vinafanya Afrika Kusini na pia kuna toa nafasi za ajira za muda kwa wakazi wa Afrika Kusini na sio Tanzania na kukosesha nafasi hiyo nchini Tanzania na wengine walienda mbali na kuwalaumu Wasanii kwanini hawafanya kazi zao Hapa Nchini na badala yake Kukimbilia Afrika Kusini. Moja ya majibu yaliyoweza Kutolewa na baadhi ya wadau ni kama ifuatavyo.

Watu wanalaumu but sio Kuwa wasanii wetu hawataki kushuti videos zao Tanzania. Diamond na wasanii wengine na some directors wa kibongo wameshaeleza Mara kadhaa Kuwa wanapenda Sana kushuti nchini tz tatizo wanakumbana na urasimu mkubwa katika kupata locations tofauti na s.africa kila kitu Ni fasta Sana wanapata na kuruhusiwa on time na kulipia gharama .

lakini bongo Inachukua muda mrefu Kama kuandika Barua kwanza sijui wizarani au Wapi na Wapi mpate kibali na mpaka mnajibiwa wiki au mwezi imeisha wakati ndani ya muda huo tayari msanii ameenda s.afrika kushuti video na anayo mkononi tayari.

Tatizo Ni Kuwa bongo ikiwemo serikali haitoi kipaumbele kwenye Sanaa kwasababu hata sera ya Sanaa ya muziki na Filamu hakuna tofauti na s.afrika kila kitu kinatambulika mpaka serikali hivyo kurahisisha mambo sababu serikali Inaingiza pato.

Jiulize hapa Tz mpaka Diamond kukubaliwa kushuti video kwenye mbuga ya wanyama au mlimani Kilimanjaro itachukuwa muda gani hata kujibiwa tu ndio au Hapana. Inshort tatizo Ni serikali sio wasanii kwasababu hata wasanii wa Filamu walishawahi kuvunjiwa kamera zao maeneo ya kivukoni kwa kushuti kwa mujibu wa Amanda kisa kushuti.

Mfano mwingine hai Ni Kuwa hata productions za Hollywood zimekuwa zikushuti some films zao Kenya na kuikwepa Tanzania makusudi kutokana na urasimu huu na pia gharama zikiwemo za kupata Vibali vya kushutia Tanzania Ni ghali kuliko Kenya na inachukuwaga muda Sana muda mrefu.
Kama serikali ya awamu ya tano inajali Sanaa , kwa hili wimbi kubwa la wasanii wa Tz kushuti videos zao S.Africa haraka Sana BASATA, wizara husika ya Sanaa na wizara ya maliasili na utalii zingeitisha kikao na wasanii kujua tatizo na kulitalitatua haraka , lakini ndio kwanza wako busy kufungia video za Kina Snura na Nay Wa Mitego huku Jambo muhimu Kama Hilo wakiliwekea pamba masikioni Kama hawalioni wakati Ni kukuza ajira na uchumi wa s.Afrika huku bongo tukizidi kudidimia both Kiuchumi na kisanaa.
Imeandikwa na Trim Saleem pamoja na Josephat Lukaza

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)